UJAMAA NA POLISI ZATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MTOAN
![]() |
Kikosi cha Polisi |
Timu za Ujamaa na Polisi zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu
fainali kwenye Kombe la Mtoano linaloendelea kwenye Dimba la Amaan.
Polisi wamewatoa El Hilal kwa penalti 5-4 baada ya kutoka
sare ya bao 1-1 kwenye dakika ya 90 ya mchezo huo uliopigwa saa 10 za jioni
jana.
Bao la Polisi limefungwa na Mohd Hassan dakika ya 16 huku bao
la El Hilal wakisawazisha dakika ya 86 kupitia Juma Makame.
Na wakati wa saa 8 za mchana Ujamaa Sports Club wakaitoa
Raskazone kwa kuifunga bao 1-0 kwenye mchezo huo.
Kwa matokeo hayo Polisi na Ujamaa wataungana na Shaba pamoja
na Hawai kucheza hatua ya nusu fainali kwenye mashindano hayo ambapo bado
haijajulikana lini na nani atacheza na nani.
Mashindano hayo yameandaliwa
na Chama cha Soka cha Wilaya ya Mjini ambapo yalishirikisha vilabu 16 kwa madaraja
tofauti vikiwemo vya ligi kuu soka ya Zanzibar, Daraja la Kwanza Taifa, Daraja
la Pili Taifa, Daraja la Pili Wilaya na Daraja la Tatu .
Comments
Post a Comment