WIKI YA JANG'OMBE BOYS HAPATOSHI, YAANZA RASMI LEO KWA KUFUNGUA MATAWI


Timu ya Jang'ombe Boys inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar imeazisha wiki yao maalum kuanzia leo Alhamis ya Septemba 7 mpaka 10, 2017 kwa kufanya shughuli mbali mbali zikiwemo za kijamii pia.

Zoezi hilo linasimamiwa na uongozi wa Friends of Boys chini ya katibu wake Alawi Haidar Foum ambapo amesema wameanzisha wiki hiyo kwaajili ya kuzidi kukaa karibu na jamii ya Kizanzibar.

"Sisi kama Jang'ombe boys kupitia  Friends of Boys tumeansisha wiki hii kwa kujiweka karibu na wadau wetu, tutazidi kufungua matawi, tutafanya usafi wa Mazingira, tutafanya harambe ya utambulisho na mwisho tutacheza mechi ya kirafiki" Alisema Alawi.

RATIBA KAMILI HII HAPA YA WIKI YA BOYS
07/09/2017. KUFUNGUWA MATAWI.
08/09/2017. USAFI WA MAZINGIRA.
09/09/2017. HARAMBEE UTAMBULISHO.
10/09/2017. MECHI YA KIRAFIKI.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE