WILAYA YA MAGHARIBI B KUANDAA KOZI YA MAKOCHA YA MSINGI


Chama cha Soka Wilaya ya Magharibi "B" wakishirikiana na Chama cha Makocha Wilaya hiyo wameandaa Kozi ya makocha ya ngazi ya msingi yani basic inatarajiwa kuanza kufanyika Septemba 20-30, 2017 katika ukumbi wa uwanja Maungani.

Kozi hiyo itahusisha zaidi ya makocha 30 wa madaraja ya Vijana pamoja na makocha wa Daraja la Pili na la Tatu kwenye Wilaya hiyo ambapo  itafundishwa na Mkufunzi Gwiji anaetambuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” Nassra Juma.

Ibrahim Makeresa ambae ni katibu wa Chama cha Makocha Wilaya ya Magharibi "B" amesema kozi hiyo ni ya siku kumi na zaidi ya makocha 30 wanatarajia kusoma.

"Tumeandaa kozi ya msingi ya makocha, na tayari tumeshapata baraka zote kutoka kwa wakubwa wetu ZFA Taifa, kozi hii itakuwa ni ya siku 10, na itafundishwa na mkufunzi Nassra Juma, hivyo nawaomba Makocha wa Wilaya yetu wajitokeze kwa wingi ili kupunguza mapungufu ya yaliyopo kwa makocha wetu, mkufunzi ametutaka makocha wasizidi 35 na wasipunguwe 30". Alisema Makeresa.

Kozi hiyo itagharimu Shilingi laki moja tu kwa kila Kocha anaehitaji kuingia katika kozi hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE