BLACK SAILORS YAZIDI KUNGARA, CHARAWE KAMA MIEMBENI CITY
Ligi kuu soka ya
Zanzibar kanda ya Unguja imeendelea tena leo kwa kupigwa michezo miwili katika
uwanja wa Amaan ambapo saa 8 za mchana Black Sailors (Mabaharia Weusi)
waliitandika Kilimani City mabao 2-0.
Mabao ya Sailors
yamefungwa na Hassan Said dakika ya 1 na Hassan Mkwabi dakika ya 89 kwa mkwaju
wa penalty baada ya mlinzi wa City Azizi Shaweji kumfanyia mazambi Iddi Idrissa.
Pia katika mchezo
huo mchezaji wa Kilimani City Humud Suleiman ameonyeshwa kadi nyekundu.
Saa 10 za jioni
Mabaharia wa KMKM wakafanikiwa kuitandika Charawe mabao 2-0.
Mabao ya KMKM
yamefungwa na Salum Akida dakika ya 60 na Mudrik Muhibu dakika ya 66.
Ligi hiyo itaendelea
tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo Saa 8:00 za
mchana Zimamoto dhidi ya Kipanga na saa 10:00 za jioni Polisi na KVZ.
Comments
Post a Comment