DK SHEIN AMTEUWA GULAM KUWA MWENYEKITI WA BTMZ
![]() |
Gulam Abdulla Rashid |
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali
Mohamed Shein, jana amefanya uteuzi kwa kumteuwa Gulam Abdulla Rashid kuwa Mwenyekiti wa baraza la Taifa la michezo Zanzibar
(BTMZ).
Uteuzi huo ameufanya Kwa mujibu wa uwezo
aliopewa chini ya kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Baraza la Michezo Namba 5 ya
2010.
Gulam ambae alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Olimpiki Tanzania (TOC) anachukua nafasi ya Sharifa Khamis (Bi Shery) ambae
alikuwa nafasi hiyo.
Comments
Post a Comment