JAN'GOMBE BOYS HOI KWA BLACK SAILORS
Mzunguko wa pili wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja
umemalizika jioni ya leo ambapo timu ya Black Sailors (Mabaharia Weusi)
wameichapa Jang’ombe Boys bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa
Amaan.
Bao pekee la Sailors lililopeleka furaha kwa kocha wao Juma
Awadh limefungwa na Abbas Peter John dakika ya 75 ya mchezo huo.
Mzunguko wa tatu wa ligi hiyo utaanza Jumamosi ya Oktoba 21
saa 8:00 za mchana katika uwanja wa Amaan kati ya Mafunzo na Taifa ya Jang’ombe
na saa 10:00 za jioni kati ya JKU na Miembeni City.
Comments
Post a Comment