KILICHOMKUTA JANA CHARAWE LEO CHAMKUTA MIEMBENI CITY KWA POLISI
Timu ya Miembeni City leo imekaribishwa kwenye ligi kuu ya
Zanzibar kanda ya Unguja baada ya kuchapwa bao 1-0 na Polisi mchezo uliochezwa
saa 10 za jioni kwenye uwanja wa Amaan.
Bao pekee la Polisi lililopeleka msiba kwa City limefungwa na
Abdallah Omar dakika ya 90 ya mchezo huo.
saa 1:00 za usiku Taifa
ya Jang’ombe imechapwa 1-0 na Zimamoto bao lililofungwa na Ibrahim Hamad Hilika dakika ya 69.
Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utakamilika kesho kwa kupigwa
mchezo mmoja saa 10:00 za jioni kati ya Black Sailors dhidi ya Chuoni.
Comments
Post a Comment