LIGI KUU SOKA YA ZANZIBAR KUANZA RASMI KESHO KUPIGWA MECHI 4
Ligi kuu Soka ya Zanzibar
msimu wa mwaka 2017-2018 unatarajiwa kuanza rasmi kesho Oktoba 3 kwa kusukumwa
michezo miwili katika uwanja wa Amaan.
Kwa upande wa Kanda ya
Unguja Mabingwa watetezi wa ligi hiyo klabu ya JKU wataanza kutetea taji lao
kwa kucheza na Mafunzo mchezo utakachezwa Saa 8:00 za mchana katika Uwanja wa
Amaan, mchezo mwengine utapigwa saa 10:00 za jioni katika uwanja huo huo wa
Amaan kati ya KMKM dhidi ya Jang’ombe Boys.
Comments
Post a Comment