LIGI KUU ZENJ YAANZA KWA KISHINDO , JKU RAHA RAHA, BOYS NA KMKM HAKUNA MBABE
Ligi kuu soka Visiwani Zanzibar kanda ya Unguja imeanza rasmi
leo kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.
Mapema saa 8 za mchana Mabingwa watetezi wa ligi hiyo JKU wameanza
vyema baada ya kuichapa Mafunzo bao 1-0 kwa bao lililofungwa na Ali Haji Said
(Zege) dakika ya 44.
Mchezo mwengine uliopigwa kiwanjani hapo majira ya saa 10 za
jioni Jangombe boys na KMKM wakaenda sare ya kufungana bao 1-1.
KMKM ndio wa kwanza kufunga bao kupitia Salum Akida dakika ya
5 ambapo bao la Boys lilifungwa na Khamis Mussa (Rais) dakika ya 25.
Comments
Post a Comment