MIEMBENI CITY YAENDELEA KUCHAPWA LIGI KUU ZENJ, JKU KAMA KAWAIDA USHINDI

Mzunguko wa Pili wa Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja umeanza leo katika uwanja wa Amaan kwa kupigwa michezo miwili.
Saa 8 za mchana mabingwa watetezi JKU wakaichapa Chuoni mabao 3-2 ambapo mabao ya JKU yamefungwa na Shomari Waziri dakika ya 12, Ali Haji Said (Zege) dakika 48 na Nassor Matar dakika ya 64, wakati mabao ya Chuoni yamefungwa na Charles Chinonso dakika ya 24 na Hamad Mshamata dakika ya 29.
Saa 10 za jioni Miembeni City ikaendelea kuchapwa katika ligi hiyo baada ya leo kupigwa na Mafunzo bao 1-0.
Bao pekee la Mafunzo limefungwa na Ali Othman dakika ya 27.ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumatatu 16/10/2017 saa 8:00 za mchana Taifa ya Jang’ombe vs Polisi na  saa 10:00 za jioni KVZ vs Zimamoto
Jumanne 17/10/2017 saa 8:00 za mchana Kipanga vs Charawe
Jumanne 17/10/2017 saa 10:00 za jioni KMKM vs Kilimani City

Jumatano 18/10/2017 saa 10:00 za jioni Black Sailors vs Jang’ombe Boys

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE