MIEMBENI CITY YAENDELEA KUCHAPWA MECHI TATU MFULULIZO, JKU WANAONGOZA LIGI KUU ZENJ KANDA YA UNGUJA
![]() |
Kikosi cha Miembeni City |
Jinamizi bado linaendelea kuwatesa timu ya Miembeni City
ambayo kwa mara ya kwanza inacheza ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja
baada ya kucheza michezo mitatu mfululizo ya awali na yote kupoteza kufuatia
kipigo cha leo cha bao 1-0 kutoka kwa JKU.
Mchezo huo umepigwa jioni ya leo katika uwanja wa Amaan
ambapo bao la JKU likifungwa na Amour Suleiman (Pwina) dakika ya 35.
Kwa matokeo hayo JKU anaongoza ligi hiyo akiwa na alama 9
kufuatia kushinda michezo yake yote mitatu ya awali baada ya kuichapa Mafunzo
1-0, kisha kuwafunga Chuoni 3-2 na leo kuwamaliza City 1-0.
Kwa upande wao Miembeni City hawana hata alama moja baada ya
kupoteza michezo yote mitatu ya mwanzo kufuatia kufungwa na Polisi 1-0, kasha wakachapwa
1-0 na Mafunzo na leo kumalizwa 1-0 na JKU.
Saa 8 za mchana leo ulipigwa mchezo mwengine kiwanjani hapo
ambapo Timu ya Taifa ya Jang’ombe (Wakombozi wa Ngambo) wametoka sare ya 1-1 na
Mafunzo.
Kwa matokeo hayo Taifa amefikisha alama 2 baada ya kufungwa
1-0 na Zimamoto, kisha wakatoka sare ya 0-0 na Polisi na leo wakatoka sare ya
1-1 na Mafunzo.
Kwa upande wake Mafunzo wamefikisha alama 4 baada ya kucheza
michezo mitatu kufuatia kufungwa 1-0 na JKU, kisha wakaichapa Miembeni City 1-0
na leo kutoka sare ya 1-1 na Taifa.
Comments
Post a Comment