MWANARIADHA GULAM KWENDA BRUNEI KUFANYA MAZOEZI MIEZI 6
![]() |
Ali Khamis Gulam |
Chama
cha Riadha Zanzibar (ZAA) kimepokea Visa ya Mwanariadha Ali Khamis Gulam ambae
anatakiwa kwenda Brunei kufanya mazoezi kwa muda wa Miezi sita.
Akithibitisha
kupokea Visa ya Mwanariadha huyo Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar
Abdulhakim Cosmas Chasama amesema chao chao kimepokea Visa ya Gulam ambapo Visa
hiyo inaaisha Januari 15, 2018.
“Tumepokea
Visa ya Mwanariadha Ali Khamis Gulam kwenda Brunei kwaajili ya mazoezi miezi
sita, atakwenda kule kwaajili ya mazoezi ili afikie viwango kwaajili ya
kushiriki Mashindano ya Jumuiya ya Madola pamoja na Olimpik, tunawaomba wadau
mbali mbali waweze kumsaidia kijana huyu ili aweze kusafiri, huduma za kule
watamuhudumia wenyewe, sisi tunaombwa tumsafirishe, kwaiyo tiketi ni kazi yetu
kuomba ili tusaidiwe mana visa yake inaisha Januari 15, 2018”. Alisema Chasama.
Mtandao
huu umemtafuta Mwanariadha Gulam ambapo amesema amepokea kwa furaha taarifa
hizo kwenda Brunei ambapo amewaahidi Wazanzibar kuyatumia vyema mazoezi hayo.
“Nimepokea
taarifa hizi kwa furaha sana, nilijitahidi ndio mana nkapata nafasi hii,
nawaahidi Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla ntaenda kuyatumia vyema Mazoezi
hayo ili niweze kufanya vyema katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola”. Alisema
Gulam.
Comments
Post a Comment