SIMBA WAANZA RASMI KUWATAFUTIA DAWA YANGA BAADA YA KUWASILI ZANZIBAR, WAPIGA MTIZI JESHINI



Kikosi cha Simba kimeanza mazoezi mepesi jioni ya leo katika uwanja wa Jeshini Migombani Mjini Unguja ambapo wapo Kisiwani hapa kwaajili ya Kambi maalum kujiandaa na mchezo wa ligi kuu soka ya Tanzania bara dhidi ya Watani wao Yanga utakaopigwa Oktoba 28, 2017 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salam.

Jumla ya wachezaji 24 wa Simba pamoja na viongozi wao wamewasili Unguja asubuhi ya leo wakitokea Jijini Dar es salam kwa furaha baada ya Jumamosi iliyopita kuwachapa 4-0 Njombe Mji kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba wataendelea kufanya mazoezi kila siku asubuhi kuanzia saa 3:00 katika uwanja wa Amaan na saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Jeshini Migombani.

Kikosi hicho kinachonolewa na Mkameroon Joseph Omog pamoja na msaidizi wake mpya Mburundi Masoud Djuma Irambona kimefikia kwenye Hoteli ya Mtoni Marine iliyopo Maruhubi Mjini Unguja.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE