ZEGE AWEKA RIKODI KUBWA LIGI KUU ZENJ
Ukiwa ni msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu Soka Zanzibar Kanda
ya Unguja, mshambuliaji wa klabu ya JKU Ali Haji Said (Zege) ameweka rikodi ya kufunga bao la mwanzo
kwenye ligi hiyo timu yake ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliopigwa
katika uwanja wa Amaan.
Nyota huyo alifunga
bao la kwanza la msimu huu wa 2017/2018 katika dakika ya 44 pambano dhidi ya
Mafunzo kabla ya wachezaji wengine hawajaanza kuandika mabao katika michezo
mengine ilifuata.
Mshambuliaji huyo ambaye
amesajiliwa na JKU kutoka JKT Ruvu Tanzania bara ilimchua dakika 44 tu
kuonyesha thamani yake ndani ya JKU.
Mara baada ya kuweka
rikodi hiyo Zege amefurahishwa mno mechi yake ya kwanza kufunga bao katika ligi
hiyo.
“Nimefurahi sana
kufunga bao, mechi yangu ya kwanza kisha nimeweka rikodi ya kufunga bao la
mwanzo, kwangu mimi ni faraja sana, wapenzi wa JKU wategemee mazuri kutoka
kwangu, kwasababu tuna umoja na upendo katika kikosi chetu cha JKU”. Alisema
Zege.
Katika msimu uliopita
bao la kwanza lilifungwa na mchezaji wa Mundu, Mwinyi Mbegu ndani ya dakika ya
22 katika pambano dhidi ya Kimbunga ambapo Mundu ilishinda mabao 2-1 ilikuwa
02/10/2016 katika uwanja wa Amaan.
Comments
Post a Comment