ZFA YAJIANDAA KUZIPELEKA ZANZIBAR HEROES KENYA, ZANZIBAR QUEENS RWANDA NA U 17 BURUNDI
Chama cha Soka Visiwani
Zanzibar (ZFA) kimepokea barua kutoka kwa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuhusu Mashindano mbali mbali wanayoandaa
Baraza hilo yakiwemo ya Chalenj kwa Wanaume na Wanawake pamoja na Mashindano ya
Vijana.
Akithibitisha kupokea Barua
kutoka CECAFA Katibu wa ZFA Mohd Ali Hilali “Tedy” amesema Zanzibar itashiriki
Mashindano yote hayo ambapo kwasasa wapo katika mchakato wa kuitafuta timu ya
Taifa ya Zanzibar kwa Wanawake (Zanzibar Queens) pamoja na Timu ya Taifa ya
Wanaume Zanzibar Heroes.
Mashindano ya CECAFA Chalenj
CUP kwa Wanawake yataanza rasmi Novemba 3 hadi 12, 2017 huko nchini Rwanda
ambapo timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Queens) itashiriki.
Kwa upande wa Wanaume
Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanatarajiwa kufanyika nchini Kenya kuanzia Novemba
25 hadi Disemba 9, 2017 ambapo timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes)
itashiriki.
Wakati huo huo kutafanyika
Mashindano ya Vijana ya CECAFA chini ya miaka 17 nchini Burundi kuanzia Disemba
12 hadi 22, 2017.
Aidha CECAFA pia wameandaa
Mashindano mengine ya Vijana ambayo yatafanyika Agost 11 hadi 25,2018 Jijini
Dar es salam ambapo timu ya Vijana ya Zanzibar U-17 pia ikitarajiwa kushiriki.
Comments
Post a Comment