ZIMAMOTO YAENDELEA KUVUTWA SHATI, KVZ YAREJEA KILELENI
Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja imeendelea tena leo kwa
kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo saa 8 za mchana Zimamoto
na Kipanga zilishindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Bao la Kipanga limefungwa na Nassor Ali wakati bao la Zimamoto
likiwekwa nyavuni na Hassan Haji.
Saa 10 za jioni katika uwanja huo KVZ wakaitandika Polisi bao 1-0
kwa lililofungwa na Salum Songoro dakika ya 79.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja katika
uwanja wa Amaan saa 10:00 za jioni kati ya Jang’ombe boys dhidi ya Chuoni.
Comments
Post a Comment