ZIMAMOTO YAPIGWA NNE,SONGORO APIGA HAT-TRICK YA KWANZA MSIMU HUU ZENJ
Mshambuliaji wa KVZ
Salum Songoro amefungua ukurasa mpya ligi kuu soka ya Zanzibar msimu huu baada
kufunga hat-trick ya kwanza katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Zimamoto
mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Amaan.
Songoro alifunga
bao hizo katika dakika ya 9, 16 na 42, Sultan Juma Kaskas alifunga bao la nne katika
dakika ya 61 huku mabao ya Zimamoto yalifungwa na Nyange Othman Denge dakika ya
63 na Idrissa Simai dakika ya 88.
Mapema saa 8 za
mchana Taifa ya Jang’ombe na Polisi walishindwa kutambiana baada ya kutoka sare
ya 0-0 katika uwanja wa Amaan.
ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumanne 17/10/2017 saa 8:00 za
mchana Kipanga vs Charawe na saa 10:00 za jioni KMKM vs Kilimani City.
Jumatano 18/10/2017 saa 10:00 za jioni Black Sailors vs Jang’ombe Boys.
![]() |
Mkurugenzi wa Ufundi wa ZFA Abdughan Msoma (Kulia) akimkabidhi Mpira Salum Songora wa KVZ baada ya kupiga Hat trick |
Comments
Post a Comment