KIKOSI CHA ZANZIBAR HEROES KINAENDELEA NA MAZOEZI
Kikosi cha timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar
(Zanzibar Heroes) kinaendelea na mazoezi yake kujiandaa na Mashindano ya CECAFA
Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017
huko nchini Kenya.
Mazoezi hayo yanayosimamiwa na kocha mkuu wa
kikosi hicho Hemed Suleiman (Morocco) yanaendelea kila siku kuanzia saa 2:00 za
asubuhi katika uwanja wa Amaan Mjini Unguja.
Mpaka sasa wachezaji waliyoanza mazoezi ni wale ambao
vilabu vyao vya Unguja huku ikiwa bado makundi mawili kutoka Kisiwani Pemba na
Tanzania Bara bado hawajajumuika na wenzao ambapo wale kutoka Pemba
wakitarajiwa kesho kuungana na wenzao.
Wachezaji waliyoanza mazoezi ni Walinda mlango Ahmed
Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman
"Wawesha" (JKU), Walinzi Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm
Mohammed "Sangula"(Jang'ombe Boys), Abubakar Ame "Luiz"
(Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya
Jang'ombe).
Viungo Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe),
Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Hamad Mshamata (Chuoni) pamoja na
washambuliaji Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe)
Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa
"Rais" (Jang'ombe boys) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).
Ambao bado hawajawasili kutoka Pemba ni Mlinda
mlango Nassor Mrisho (Okapi), Viungo Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi) na
Mbarouk Marshed (Super Falcon) pamoja na mshambuliaji Mwalimu Mohd (Jamhuri).
Wachezaji ambao wanatokea ligi kuu soka Tanzania
bara ambao bado hawajajumuika na wenzao ni Walinzi Abdallah Haji
"Ninja" (Yanga), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji
Mwinyi Ngwali (Yanga), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam), Viungo Mudathir
Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar) na Suleiman
Kassim "Seleembe" (Majimaji) pamoja na washambuliaji Kassim Suleiman
(Prisons), Matteo Anton (Yanga) na Seif Rashid Abdallah “Karihe” (Lipuli).
Kiungo mshambuliaji Feisal Salum (JKU) nae bado
hajajiunga na wenzake kufuatia kuwepo kambi ya timu ya Taifa ya Vijana Tanzania
wenye umri chini ya miaka 23 Kilimanjaro Warriors huku mshambuliaji Ali Yahya anaecheza
soka nchini Spain nae bado hajawasili Zanzibar.
Comments
Post a Comment