KOCHA MOROCCO AMUONGEZA SEIF KARIHE ZANZIBAR HEROES
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar
(Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman (Morocco) amemuongeza kwenye kikosi Mshambuliaji
wa Lipuli ya Iringa Seif Rashid Abdallah (Karihe) ili kuzidi kuipa nguvu timu
hiyo itakayokwenda Kenya katika Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa
kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017.
Katika uteuzi wa awali wa wachezaji 30 Karihe
hakuitwa lakini kocha Morocco amelazimika kumuongeza mshambuliaji huyo na
atakuwa mchezaji wa 31 kuitwa katika kikosi cha awali huku Morocco akisema si
kosa kwa timu ya Taifa kupunguza au kuongeza mchezaji wakati wowote tu ikiwa
bado haijaenda katika Mashindano.
“Hii ni timu ya Taifa wakati wowote unamwita
mchezaji au unamtoa kutokana na mahitaji yako, nimelazimika kumuongeza Karihe
kwasasa ataungana na wenzake 30 wale wa awali”. Alisema Morocco.
Karihe ambae ni mchezaji wa zamani wa Azam FC
ataungana na wenzake Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi), Mohammed Abdulrahman
"Wawesha" (JKU), Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe
Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU), Abdulla Kheir
"Sebo" (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).
Wengine ni Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe),Mudathir
Yahya (Singida United), Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi), Mohd Issa
"Banka" (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Mbarouk
Marshed (Super Falcon), Ali Yahya (Academy Spain), Hamad Mshamata (Chuoni), Suleiman
Kassim "Seleembe" (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons)
Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya
Jang'ombe)
Feisal Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ), Khamis
Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri) na Ibrahim
Hamad Hilika (Zimamoto).
Comments
Post a Comment