MIEMBENI CITY BADO MAJANGA, AFADHALI WAMEFUNGWA LAKINI WAMEWEKA RIKODI YA KUFUNGA BAO


Timu ya Miembeni City bado inaendelea kufanya vibaya katika ligi kuu soka ya Zanzibar baada ya leo kufungwa 2-1 na klabu ya KVZ katika mchezo uliopigwa saa8 za mchana katika uwanja wa Amaan.

Licha ya kufungwa City lakini wameweka rikodi kwa upande wao baada ya kupata bao moja lililofungwa na Nahodha wao Habibu Ali dakika ya 56 kwa njia ya penalty ambapo City waliwahi kufika dakika 450 kwa michezo mitano pasipo kushinda alau bao moja.

Mabao ya ushindi ya KVZ yote yamefungwa na mshambuliaji Salum Songoro dakika ya 39 na 42.

Saa 10 za jioni Taifa ya Jang'ombe wakatoka sare ya 1-1 na Chuoni ambapo bao la Taifa limefungwa na Abdul Azizi Makame (Abui) dakika ya 16 huku bao la Chuoni likifungwa na Charlses Chinonso dakika ya 26.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja katika uwanja wa Amaan saa 10:00 za jioni kati ya Kipanga na JKU.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE