MZEE ZAM AULA CECAFA

Makamo wa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA Unguja) Mzee Zam Ali ameteuliwa kuwa mjumbe katika kamati itakayosimamia Mashindano ya Chalenj CUP yaliyoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Mashindano ambayo yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya.

CECAFA wamemteuwa Mzee Zam kwakuwa ni mzowefu katika Mashindano hayo ambapo ni Mzanzibar pekee kwenye kamati hiyo.

Wengine waliochaguliwa katika kamati hiyo ni Mutasim Gafar (Sudan), Abdigaan Arab Said (Somalia), Jacob Odundo (Kenya), Ashinafi Ejigu (Ethiopia), Aimable Habimana (Burundi), Rogers Byamukama (Uganda), Ajong Domasio Ajong (Sudan ya Kusini) na Ahmed Mgoyi (Tanzania Bara).


Wengine ni Sunday Kayuni (Tanzania Bara), Mossi Yussuf (Burundi), Celestine Ntangugira (Rwanda), Yigzaw Ambaw (Ethiopia), Bernard Mfubusa (Burundi), Maxim Itur (Kenya), Rogers Mulindwa (Uganda), Bonny Mugabe (Rwanda), Gishinga Njoroge (Kenya), Amir Hassan (Somalia) na Nicholas Musonye (Kenya).

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS