TIMU ZITAKAZOSHIRIKI KOMBE LA MAPINDUZI 2018 ZAWEKWA HADHARANI, AZAM, YANGA, SIMBA NA TAIFA YA JANG'OMBE KAMA KAWAIDA, SHABA NA MLANDEGE NAO MZIGONI

Kamati inayosimamia mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup 2018) inaendelea na matayarisho ya michuano hiyo huku timu 10 zinatarajiwa kushiriki msimu huu.

Mashindano hayo yatashirikisha timu 3 kutoka Tanzania Bara ambazo ni Azam (Mabingwa Watetezi), Simba na Yanga ambapo Unguja zitashiriki timu 4 ambazo ni JKU, Zimamoto, Taifa ya Jang'ombe na Mlandege huku timu mbili kutokea Pemba Shaba na Jamhuri na timu moja kutoka nje ya Tanzania bado haijajulikana lakini itatokea Kenya au Uganda.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi mwishoni mwa mwezi Disemba na fainali itapigwa Januari 13, 2018.

Wajumbe wa Kamati wanaosimamia Mashindano hayo Mwenyekiti ni Sharifa Khamis, huku Makamo Mwenyekiti Gulam Rashid, Katibu Khamis Abdalla Said huku Wajumbe wakiwa Issa Mlingoti Ali, Dk. Ally Saleh Mwinyikai,  Ali Khalil Mirza, Khamis Mzee Ali, Ravia Idarous Faina, Ali Mohammed, Mohammed Ali Hilali (Tedy) na Juma Mmanga.
Khamis Abdallah Said katibu wa kamati ya Mapinduzi cup 2018

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE