WACHEZAJI WOTE WANAOCHEZA LIGI KUU BARA HUENDA WAKAACHWA ZANZIBAR HEROES BAADA YA KLABU ZAO KUWABANIA

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), ambao wanacheza ligi kuu soka Tanzania bara huenda waachwa katika kikosi hicho kutokana na kutopewa ruhusa na vilabu vyao kujiunga na timu hiyo ya Taifa mpaka ligi kuu bara itakapokwenda mapumziko.

Kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman (Morocco) amesema kutokana na kutopewa ruhusa wachezaji hao huenda wakawasamehe na badala yake wakawachagua wachezaji wengine wanaocheza soka hapa hapa Zanzibar.

Morocco amesema ikifika Novemba 15 ikiwa bado wachezaji hao hawajawasili kambi ya Heroes watalazimika kuwaacha na kuongeza nguvu kwa vijana wanaocheza vilabu vya Zanzibar kwani hawawezi kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na kambi siku chache kabla hawajasafiri.

"Tumeshaanza mazoezi tangu juzi, lakini uhakika wa kuwapata wachezaji wanaocheza ligi ya bara ngumu, tumewasiliana na vilabu vyao lakini wametuambia wachezaji hawaruhusu kujiunga na sisi mpaka ligi isimame Novemba 19, nasisi tunataka kuondoka Novemba 22, sasa itakuwa muda hawajapata kukaa na wenzao kwasababu pengine wafike Zenj Novemba 20 au 21 sasa apo bora tuwasamehe na tuwaite wengine wanaocheza hapa hapa Zanzibar". Alisema Morocco.

Wachezaji waliyoitwa awali katika kikosi cha Zanzibar Heroes ambao wanatokea ligi kuu soka Tanzania bara ni Walinzi Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam), Viungo Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar) na Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji) pamoja na washambuliaji Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga) na Seif Rashid Abdallah “Karihe” (Lipuli).


Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE