WAZANZIBAR WAWILI WALOITWA TIMU YA TAIFA TANZANIA WAENDA KAMBINI LEO AMBAO NI FEI TOTO NA JAILANI
![]() |
Fesal Salum kushoto na kulia Mohd Jailan |
Benchi la Ufundi la timu za taifa za vijana, limeita wachezaji 35 kwa ajili ya kambi yenye lengo la mchujo kutafuta kikosi imara cha timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 ambapo miongoni mwa wachezaji hao wawili wanatoka ligi ya Zanzibar ambao ni Wazanzibar.
Kocha Msaidizi wa timu hizo, Oscar Mirambo alitangaza majina hayo Juzi Novemba 03, mwaka huu huku akisema wanahitaji vijana wasiozidi 25 kwenye kikosi ambao leo Jumapili wameanza kambi ya siku 10.
Wachezaji aliowaita ni makipa Metacha Mnata (Azam FC), Joseph Ilunda (JKT Ruvu), Liza Mwafwea (Tanzania Prisons).
Wengine ni Cleotas Sospter (Yanga); Idrissa Mohammed, Bakari Kijuji (Yanga), Joseph Prosper (Azam), Masoud Abdallah (Azam), William (Ruvu Shooting), Yussuph Mhilu (Yanga), Adam Salamba (Stand United), Omary Mponda (Ndanda) na Stanley Angeso (Stand United).
Pia wamo Eliud Ambokire (Mbeya City), Emmanuel Kakuti (Mbeya City), Medson Mwakatunde (Mbeya City), Daruweshi Shaliboko (Ashanti Unted), Abbas Kapombe (Azam/Ndanda), Ismail Aidan (Mtibwa Sugar), Salum Kihimbwa (Mtibwa Sugar), Hassan Mganga (Mtibwa Sugar) na Award Salum (Njombe Mji).
Wengine Awesu Ally (Mwadui), Salum Chuku (Singida United), Yahya Zayd (Azam), Emmanuel Martin (Yanga), Geofrey Mwashiuya (Yanga), Ayoub Masoud (Ndanda), Baraka Majogoro (Ndanda), Mohammed Habib (Miembeni city), Yussuf Mlipili (Simba), Agathon Mapunda (Njombe Mji), Faisal Abdallah (JKU) na Yussuph Kagoma (Singida United).
![]() |
Mohd Jailan |
Comments
Post a Comment