CECAFA YAWAHOFIA ZANZIBAR HEROES, WASEMA WAPIMWE YAWEZEKANA WANATUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
yaingiwa na hofu kwa kiwango bora wanachoonyesha timu ya Taifa ya Zanzibar
(Zanzibar Heroes) katika Mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup yanayoendelea
nchini Kenya.
Hofu hiyo imekuja jioni ya leo katika uwanja wa Kenyatta
Mjini Machakos mara baada ya kutoka sare ya 0-0 na Wenyeji Kenya na kupelekea
Zanzibar kutinga moja kwa moja nusu fainali wakiwa na alama 7 wakiongoza kundi
lao A lenye Mataifa kama Kenya, Libya, Rwanda na kaka zao Tanzania bara.
Baadhi ya wajumbe wa CECAFA wakiongozana na wakaguzi wanaopinga
dawa za kuongeza nguvu Michezoni (World Anti Doping) walikwenda kwenye vyumba
vya kubadilisha nguo vya Zanzibar Heroes kwa kusema haiwezekani timu ya
Zanzibar icheze michezo mitatu mfululizo bila ya kuonekana kuchoka.
“Mechi tatu mfululizo Zanzibar wanacheza kwa kiwango bora,
tena wachezaji wao ndo wale wale kila siku wanaoanza labda abadilike mmoja tu, itakuwa
wanatumia dawa za kuongeza nguvu lazima wachunguzwe”. Alisema mmoja wa Afisa kutoka
World Anti Doping.
Uongozi wa Zanzibar Heroes ukakubali wachezaji wake kwenda
kupimwa kama kweli wanatumia dawa za kuongeza nguvu au kiwango chao tu,ukatokea
mtafaruku baina yao wenyewe viongozi wa CECAFA na mwisho wakakubali kuwaachia
wachezaji hao waende zao wachezaji ambao walishangazwa mno kusikia kuwa
wanatumia dawa.
“Hahahahah, ati tunatumia dawa kwakuwa tunacheza na timu
zenye wachezaji wakubwa ki umbo kisha wanashindwa kutufunga, sisi tumekuja hapa
Kenya kufanya kazi tuloagizwa na viongozi wetu, hata kama tumekuja kwa Basi
lakini tunajituma kuhakikisha tunafanya vyema, wasishtuke huu ni urojo tu wa
Zanzibar si chengine, sisi kazi kazi tu hatumuagalii mtu usoni”. Alisema mmoja
wa wachezaji wa Zanzibar.
Comments
Post a Comment