DABI YA TANZANIA KATI YA ZANZIBAR HEROES NA KILIMANJARO STARS GUMZO KENYA, HAPATOSHI KESHO
Ndugu wa wawili wa Tanzania kesho Alhamis watakutana katika Soka kwenye Mashindano ya kuwania ubingwa wa Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA SENIOR CHALLENGECUP), kati ya timu ya Taifa ya Zanzibar “Zanzibar Heroes” dhidi ya Tanzania bara “Kilimajanjaro Stars” mchezo utakaopigwa majira ya saa 8:00 za mchana katika Uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya.
Huu ni mchezo wa pili kwa kila timu kufuatia Heroes jana
kushinda mabao 3-1 dhidi ya Rwanda wakati Kilimanjaro Stars walitoka sare ya
0-0 dhidi ya Libya katika mchezo wao wa awali, hivyo mechi hiyo ni muhimu kwa
kila upande kupata alama tatu ili kujiwekea matumaini ya kucheza nusu fainali
ambapo katika kundi lao A kuna timu 5 zinalazimika timu 2 kwenda hatua hiyo.
Katika kundi hilo A Kenya wanaongoza wakiwa na pointi nne baada ya kuifunga Rwanda mabao 2-0, kisha wakatoka 0-0 na Libya wakati Zanzibar Heros wakishika nafasi ya pili kwa alama zake tatu huku Libya wakishika nafasi ya tatu kwa alama zao mbili ambapo Kilimanjaro Stars wakishika nafasi ya nne kwa point yao moja na Rwanda hawana alama wakikamata nafasi ya 5.
Kilimanjaro Stars imetwaa mara tatu tu taji hilo, 1974, 1994
na mwaka 2010 wakati Zanzibar wenyewe walitwaa taji hilo mara moja tu mwaka
1995.
Uganda
ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo tangu mwaka 1971, wakiwa
wamelitwaa mara 14, wakifuatiwa na Kenya mara sita, Ethiopia mara nne na
Tanzania bara mara tatu.
Uganda, The Cranes pia ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji la michuano hiyo mwaka 2015 nchini Ethiopia wakiwafunga Rwanda 1-0 kwenye fainali mjini Addis Ababa, wakati mwaka jana michuano hiyo haikufanyika kwa sababu ya kukosa nchi mwenyeji.
Comments
Post a Comment