HAJI MWINYI NA WENZAKE WAWILI KUUKOSA MCHEZO WA KESHO ZANZIBAR VS UGANDA
Mlinzi wa kushoto Mwinyi Haji Ngwali ataukosa mchezo wa kesho
wa Zanzibar wakiwavaa mabingwa watetezi Uganda.
Zanzibar Heroes watakipiga na Uganda katika mchezo wa nusu
fainali ya pili kwenye mashindano ya Cecafa Senior Challenge Cup, mchezo
utakaopigwa saa 9:00 za Alaasiri kwenye uwanja wa Moi uliopo Kisumu.
Mwinyi ataukosa mchezo huo mara baada ya kupigwa kadi mbili
za njano katika michezo miwili mfululizo iliyopita ukiwepo waliotoka sare ya
0-0 na Kenya na ule waliofungwa 1-0 na Libya ambapo kanuni ya mashindano hayo
mchezaji akipewa kadi mbili mfululizo za njano katika michezo miwili mfululizo
atalazimika kuukosa mchezo unaofuata.
Nafasi ya Mwinyi kesho itazibwa na Adeyum Ahmed Seif ambae
pia ni mzoefu katika Mashindano hayo ya Cecafa.
Mbali ya Mwinyi pia Zanzibar Heroes itawakosa huduma za nyota
wake wengine akiwepo mfungaji wao Kassim Suleiman Khamis pamoja na kiungo Amour
Suleiman “Pwina” ambao wote ni majeruhi.
“Mwinyi hatocheza ana kadi 2 za njano, lakini pia Kassim na
Amour nao tutawakosa kutokana na majeruhi”. Alisema Kocha wa Zanzibar Heroes Hemed
Suleiman (Morocco).
Lakini kwa upande wa timu ya Uganda kesho itawakosa nyota
wake wawili muhimu akiwemo Mulema Isaack na Awany Tinoethy ambao wote walipewa
kadi mbili za manjano katika michezo miwili mfululizo iliyopita.
"Ni mechi ngumu nawajua sana Zanzibar lakini na
sisi tutawaonyesha kama tunataka kulitetea kombe letu". Alisema Moses
Basena kocha mkuu wa Uganda.
Comments
Post a Comment