JKU KUCHEZA NA WAZAMBIA, ZIMAMOTO NA WA ETHIOPIA, YANGA NA SHELISHELI WAKATI SIMBA NA WA DJIBOUTI
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) leo limetoa ratiba ya
awali ya Kombe la Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho barani humo huku
wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano hayo kuwajua wapinzani wao ambapo
michezo ya awali yote wataanzia nyumbani Zanzibar katika uwanja wa Amaan.
JKU ambao ndio mabingwa watetezi wa Zanzibar wamepangwa
kucheza na Zesco United ya Zambia kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa huku
Zimamoto ambao ni makamo Bingwa wa Zanzibar watacheza na Wolaitta Dicha ya Ethiopia.
Na kwa upande
wa Wawilishi wa Tanzania bara katika Mashindano ya Klabu Bingwa, Yanga watacheza
na St
Louis ya Shelisheli huku Simba watakipiga na Gendamarie ya Djibouti
kwenye kombe la Shirikisho.
Comments
Post a Comment