NYOTA WA 4 WA ZANZIBAR WAPIMWA MKOJO NA WORLD ANTI DOPING AGENCY KUHUSU KUTUMIA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU
Mawakala wa kupinga utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu
Michezoni nchini kupitia tawi lao nchini Kenya (World Anti-Doping Agency “WADA”)
kwa kushirikiana na Baraza la Vyama vya Michezo Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA) linawasi wasi na wachezaji
wanne wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kutumia dawa hizo.
Wachezaji hao ni Kiungo Mohd Issa “Banka”, Fesal Salum “Fei
Toto” na Washambuliaji Ibrahim Hamad Hilika na Suleiman Kassim “Seleembe”.
Hofu hiyo imekuja kwenye Mashindani ya Cecafa Senior Chalenj
Cup jioni ya leo katika uwanja wa Kenyatta Mjini Machakos mara baada ya kutoka
sare ya 0-0 na Wenyeji Kenya na kupelekea Zanzibar kutinga moja kwa moja nusu
fainali wakiwa na alama 7 wakiongoza kundi lao A lenye Mataifa kama Kenya,
Libya, Rwanda na Tanzania bara.
WADA na CECAFA wameingiwa na wasi wasi kutokana na kiwango
bora walichoonyesha Zanzibar katika Mashindano hayo huku ikiwaongoza mataifa
kama Libya, Rwanda, wenyeji Kenya na Tanzania Bara.
WADA na CECAFA baada ya kumaliza mchezo wa leo waliwafata
wachezaji hao katika vyumba vya kubadilisha nguo lakini hawakufanikiwa kuwapima
jambo ambalo limepelekea kuwafata mpaka kambini kwao kwenye Hoteli ya Garden
iliyopo Mjini Machakos nchini Kenya.
Awali walisema Wachezaji wa Zanzibar wana mashaka nao na
jinsi wanavyocheza si bure, hivyo baadae wakawataja wachezaji hao wanne akiwemo
kiungo kinda Fesal Salum “Fei Toto” ambae leo amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo
wa leo kati ya Zanzibar na wenyeji Kenya ulomalizika 0-0.
Tangu kuanza Mashindano haya mwaka huu Zanzibar inaongoza
kutoa wachezaji bora wa mchezo yani Men of the Match ambapo mchezo wa awali
Zanzibar Heroes waliichapa Rwanda mabao 3-1 huku mchezaji bora akitajwa kuwa
Mohd Issa “Banka”, mchezo wa pili Zanzibar waliwafunga Tanzania bara mabao 2-1
na mchezaji bora wa mchezo akawa Ibrahim Hamad “Hilika” na leo Zanzibar 0-0
Kenya mchezaji bora pia katoka Zanzibar Fesal Salum.
Hivyo wale wote nyota wa mchezo wa Zanzibar wameorodheshwa
katika kundi hilo.
Kwasasa zoezi hilo la kupimwa mkojo kwa wachezaji hao
linafanywa hapa Garden Hotel Machakos, endelea kufatilia Blog hii utajua zoezi
hilo linavyokwenda.
Ndio kawaida ya Waswahili wakikuona unaelekea kwenye mafanikio basi atakuekea kikwazo tu
ReplyDeleteNdio kawaida ya Waswahili wakikuona unaelekea kwenye mafanikio basi atakuekea kikwazo tu
ReplyDelete