NYOTA WA ZANZIBAR HEROES NA SINGIDA UNITED BAADA YA KUTANGAZWA KUWA MCHEZAJI BORA ASEMA WALOMCHAGUA HAWAJAKOSEA
Siku moja mara baada ya kutangazwa kuwa mchezaji Bora wa
Mwezi Novemba, 2017 wa Ligi Kuu Soka ya Tanzania Bara msimu wa 2017/2018
Mudathir Yahya amesema amezipokea kwa furaha taarifa hizo kwani yeye alistahiki
kuipata nafasi hiyo.
Mudathir amesema alikuwa akimuomba Mwenyezi Mungu kila siku
ili Mwezi huo achaguliwe yeye kwani alionyesha kiwango cha hali ya juu kabisa.
“Namshukuru Mwezi Mungu kwa kunijaalia kuchaguliwa mimi kuwa mchezaji
bora wa Mwezi, nilikuwa namuomba Mungu kila siku nikisali ili nichaguliwe mimi,
namshkuru kocha wangu Hans pamoja na wachezaji wenzangu wote wa Singida United,
na pia nilistahiki kuchaguliwa kwani nilicheza vizuri sana mwezi Novemba”.
Alisema Mudathir.
Mudathir alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili,
Beki Asante Kwasi wa Lipuli ya Iringa na Mshambuliaji Danny Usengimana pia wa
Singida United, alioingia nao fainali ya kuwania nafasi hiyo.
Jopo la makocha na wachambuzi wa habari za michezo walipendekeza
jina la Mudathir kutokana na mchango alioutoa kwa timu yake katika mechi tatu
ambazo walicheza kwenye uwanja wa Namfua Singida ambazo zote timu yake ya
Singida United iliibuka na ushindi.
Singida United ilitoka 0-0 na Yanga, iliifunga Mbeya City mabao
2-1 na pia iliifunga Lipuli bao 1-0, ambapo Mudathir anayecheza nafasi ya
kiungo alicheza dakika zote 270 sawa na michezo mitatu na hakuwa na kadi
yoyote.
Kwasasa Mudathir yupo Machakos nchini Kenya akiitumikia timu yake
ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwenye Mashindano ya Cecafa Senior
Chalenj Cup yanayoendelea nchini Kenya ambapo Heroes inaendelea kufanya vyema
kwenye kundi lake A.
Comments
Post a Comment