SARE DHIDI YA LIBYA YAMSONONESHA ERASTO NYONI
NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania
Bara (Kilimanjaro Stars) Erasto Edward Nyoni anaonekana kusononeshwa na sare
waliyotoka na Libya baada ya kusema kuwa walitegemea kushinda lakini haikuwa
bahati kwao.
Katika mchezo huo wa jana, wa kombe la CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP uliopigwa katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, Kilimanjaro walipata kazi ngumu mbele ya Waarabu wa Libya
na kulazimika mchezo huo kutoka sare ya 0-0.
“Tulitegemea kupata ushindi lakini
imeshindikana, Libya ni wazuri lakini tunashkuru Mungu kupata alau hiyo point
moja”. Alisema Nyoni.
Mchezo wa pili Kilimanjaro Stars
itacheza na ndugu zao Zanzibar Heroes siku ya Alhamis ya Disemba 7 saa 8:00 za
mchana katika uwanja wa Kenyatta
.
Comments
Post a Comment