YULE MGOLI GOLI WA ZANZIBAR HEROES ANAETAKIWA NA SIMBA KUKOSA MICHEZO YOTE CHALENJ CUP
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Kassim Suleiman Khamis anatarajiwa kukosa michezo yote iliyosalia katika Mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup yanayoendelea nchini Kenya.
Mshambuliaji huyo anaecheza klabu ya Tanzania Prisons kwenye
ligi kuu soka Tanzania Bara ameumia mguu wake wa kulia baada ya kugongana na Daniel
Lyanga wa Kilimanjaro Stars katika mchezo ambao Zanzibar Heroes walipoichapa
Tanzania Bara mabao 2-1.
Daktari Mkuu wa Zanzibar Heroes, Mohd Said alithibitisha taarifa hizo za kukosa huduma ya mshambuliaji huyo.
“Awali tulitegemea angeweza kuipata nusu fainali na mchezo wa
mwisho, lakini mpaka sasa dalili hiyo haipo tena na atalazimika kukosa
mashindano yote haya ukiwemo mchezo wa kesho dhidi ya Uganda na ule wa mwisho”.
Kassim ndie kinara wa kufunga mabao kwa upande wa Zanzibar baada ya kufunga mabao mawili yote akitokea benchi katika michezo Heroes iliposhinda 3-1 dhidi ya Rwanda na ule wa 2-1 dhidi ya Tanzania bara na kupelekea vilabu vingi ikiwemo Simba kuhitaji huduma yake.

Comments
Post a Comment