ZANZIBAR HEROES IKIIFUNGA KENYA KESHO INATINGA NUSU FAINALI KWA KISHINDO
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) ndio kinara wa
kundi lao A wakiwa na alama sita katika Mashindano ya kuwania
ubingwa wa Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA
SENIOR CHALLENGECUP) Mashindano ambayo yanaendelea nchini Kenya.
Mchezo wa awali Zanzibar Heroes iliichapa Rwanda mabao 3-1
kwa magoli yalofungwa na Mudathir Yahya, Mohd Issa (Banka) na Kassim Suleiman
huku mchezo wa pili jana waliifunga Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) mabao 2-1
kwa msaada wa mabao yalofungwa na Kassim Suleiman na Ibrahim Hamad Hilika
ambapo kesho Jumamosi watacheza mchezo wa tatu dhidi ya wenyeji Kenya.
Endapo kesho Heroes wakifanikiwa kuwafunga Kenya watajihakikishia
kutinga hatua ya nusu fainali kwani watafikisha alama 9, alama ambazo
hazitoweza kufikiwa na timu yoyote katika kundi hilo.
Katika Mashindano ya mwaka huu Heroes inaonekana kuwavutia
wapenzi wengi kutokana na soka safi wanalolitandaza na kuonyesha vipaji
walivyonavyo, jambo ambalo limepelekea Wakenya wengi hapa Mjini Machakos kusema
kuwa timu yao wanayoipenda ni Zanzibar.
Comments
Post a Comment