ZANZIBAR HEROES WAPO TAYARI KUWAVAA RWANDA KESHO
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa awali kesho Disemba 5 wa kombe la CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP dhidi ya Rwanda katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, pambano litakalopigwa majira ya saa 8:00 za mchana.
Zanzibar Heroes wanashuka dimbani huku kikosi kizima kikiwa katika hali nzuri ambapo ripoti ya Kocha imesema kwamba hakuna mchezaji yoyote ambaye ana majeraha yatakayomzuia kucheza mchezo huo muhimu kwao.
“Kikosi kizima kipo sawa hatuna majeruhi yoyote, na tumefanya mazoezi mepesi katika uwanja Machakos Girl High School kwa ajili ya mchezo huo, tunawaheshimu Rwanda hasa wakiwa katika Katika Mashindano haya ni timu nzuri na tunatarajia kushuhudia mchezo mzuri kwa kila upande”. Alisema Kocha mkuu Hemed Suleiman (Moroco).
Katika mchezo huo Heroes inawategemea zaidi viungo wake
mahiri Mudathir Yahya wa Singida United na Mohd Issa "Banka" wa Mtibwa
Sugar.
Benchi la ufundi la Hereos linaongozwa na
Hemed Suleiman “Morocco” (Kocha Mkuu), Hafidh Muhidin (Msaidizi), Ali Suleiman
“Mtuli” (Msaidizi), Abdulwahab Dau (Meneja), Saleh Ahmed “Machupa” (Kocha wa
Makipa)na Abrahmani Ali (Mtunza vifaa).
Wachezaji 24 waliochaguliwa kuwakilisha
kikosi hicho ni :-
WALINDA
MLANGO
Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya
Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha"
(JKU).
WALINZI
Abdallah Haji "Ninja" (Yanga),
Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe
Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali
(Yanga), Issa Haidar "Mwalala" (JKU), Abdulla Kheir "Sebo"
(Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).
VIUNGO
Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul
Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa
"Banka" (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman "Pwina" (JKU) na
Hamad Mshamata (Chuoni).
WASHAMBULIAJI
Suleiman Kassim "Seleembe"
(Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons), Feisal Salum (JKU), Khamis
Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah
“Karihe” (Lipuli) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).
Comments
Post a Comment