ZANZIBAR HEROES YAWASILI SALAMA MACHAKOSI KENYA, TAYARI KUCHEZA CHALENJ CUP
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imefika
salama katika Jiji la Machakos nchini Kenya tayari kuanza Mashindano ya CECAFA
Chalenj Cup ambayo yanatarajiwa kuanza kesho kutwa Jumapili Disemba 3, 2017.
Jumla ya msafara wa watu 41 wakiwemo wachezaji 24 umewasili
jioni ya leo na wamefikia katika Hoteli ya Garnen Hotel iliyopo Machakosi.
Mkuu wa Msafara huo Khamis Ali Mzee amesema
wamepokelewa vizuri na uongozi wa CECAFA hivyo imezidi kuwapa ari ya kufanya
vizuri katika Mashindano hayo.
“Tunashukuru tumefika salama hapa Kenya, safari
ilikuwa ngumu kiasi lakini tunashukuru uongozi wa CECAFA kuja kutupokea,
tunaimani vijana watafanya vyema katika Mashindano”. Alisema Mzee.
Heroes wataanza kucheza mchezo wao wa awali Jumanne
saa 8:00 za mchana dhidi ya Rwanda.
Benchi la ufundi la Hereos linaongozwa na Hemed
Suleiman “Morocco” (Kocha Mkuu), Hafidh Muhidin (Msaidizi), Ali Suleiman “Mtuli”
(Msaidizi), Abdulwahab Dau (Meneja), Saleh Ahmed “Machupa” (Kocha wa Makipa)na Abrahmani
Ali (Mtunza vifaa).
Wachezaji 24 waliochaguliwa kuwakilisha kikosi hicho ni :-
WALINDA MLANGO
Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho
(Okapi) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU).
WALINZI
Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga
(Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh
"Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Issa Haidar
"Mwalala" (JKU), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam) na Ibrahim
Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).
VIUNGO
Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya
Jang'ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa
Sugar), Amour Suleiman "Pwina" (JKU) na Hamad Mshamata (Chuoni).
WASHAMBULIAJI
Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji), Kassim Suleiman
(Prisons), Feisal Salum (JKU), Khamis Mussa "Rais"
(Jang'ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah “Karihe” (Lipuli) na
Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).
Comments
Post a Comment