MZEE ZAM WA ZANZIBAR APEWA FUPA NA CAF


Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Mzee Zam Ali kutoka Zanzibar kuwa Kamishna wa mchezo nambari 50 wa kombe la shirikisho kati ya FC Platinum ya Zimbabwe dhidi ya Club Desportivo 1 de Agosto ya Angola mchezo utakaopigwa 20 au 21 ya February, 2018 huko Zimbabwe.

Mzee Zam atawasimamia Waamuzi wa Afrika ya Kusini watakaochezesha mchezo huo akiwemo muamuzi wa kati Christopher Harrison, akisaidiwa na muamuzi namba moja Sandile Dilikane na muamuzi namba mbili Thembisile Theophilus huku Muamuzi wa akiba akiwa Tinyiko Victor Hlungwani.

“Nimefurahi CAF kuendelea kuwa na imani na mimi kwani wananijua vyema hasa hivi karibuni nilikuwa Kamishna katika Mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup yaliofanyika nchini Kenya, mimi ni mzoefu kuchaguliwa kwenye shughuli za soka kama hizi katika Mashindano mbali mbali”. Alisema Mzee Zam.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS