SERIKALI ITAWACHUKULIA HATUA ZFA IKITHIBITIKA KUWA WAO NI SABABU YA KUONDOSHWA KARUME BOYS CECAFA BURUNDI
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya Vijana Sanaa Utamaduni na
Michezo leo imetoa taarifa na ufafanuzi juu ya timu yake ya Taifa ya Vijana
chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) ambayo imeondolewa kwenye Mashindano ya
CECAFA U-17 yanayoendelea nchini Burundi.
Katibu
mkuu wa Wizara hiyo Omar Hassan (King) ametoa ufafanuzi huo mbele ya Waandishi
wa Habari kuhusu kadhia hiyo iliyotea kwa Vijana wa Zanzibar huko nchini
Burundi ambapo amesema ikithibitika kuwa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) wao ndio
wenye makosa mpaka Karume Boys wakaondoshwa katika Mashindano basi wajiwajibishe
wenyewe kwa kujiuzulu.
"Kama itakuwa kosa lao ZFA na kama Mimi nimo ZFA basi ntakaa pembeni, naamini na wao wenyewe watatumia busara ya hali ya juu kukaa pembeni".
Zanzibar
iliondolewa katika Mashindano hayo na kupigwa faini kwa kosa la kuorodhesha
wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo kanuni ya Mashindano hayo
iliwataka wachezaji waliozaliwa kuanzia 01/01/2002 huku Zanzibar ikuwapeleka
wachezaji 12 waliozaliwa 2001 jambo ambalo ZFA wamesema hawana taarifa kama
wachezaji walotakiwa waliozaliwa 2002 ambapo wao walijuwa walokuwa na umri
chini ya miaka 17 hivyo hata walozaliwa 2001 ikiwa bado hawajafika miaka 17
walifikiri wanaruhusiwa ndio mana wakaenda nao ambapo katibu Mkuu wa CECAFA
Nicholaus Musonye alisema kuwa ZFA walitumiwa ufafanuzi wa umri kwenye Barua
Pepe labda hawazisomi tu.
Kutokana
na makosa hayo Karume boys imepewa adahabu tatu ikiwemo
kuondolewa mashindanoni, inaambatana na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni) zinazotakiwa
kulipwa na Chama cha Soka la Zanzibar (ZFA), ambapo fedha hizo zitafidia
gharama za tiketi, malazi na chakula ya timu katika kipindi chote walichokaa
Burundi huku adhabu ya tatu ikiwa kufungiwa kutoshiriki mashindano yanayoendeshwa
na CECAFA hadi hapo watakapolipa faini hiyo ambayo inatakiwa kurudishwa FIFA.
Karume boys ilikuwa icheze juzi Jumapili mchezo wake wa kwanza dhidi ya Sudan katika uwanja wa Gitega mchezo ambao haukuchezwa baada ya Sudan kupeleka malalamiko yao kwa CECAFA na mchezo huo ukafutwa ambapo Vijana hao wanategemea kurejea nyumbani leo majira ya saa 2 za usiku.
Karume boys ilikuwa icheze juzi Jumapili mchezo wake wa kwanza dhidi ya Sudan katika uwanja wa Gitega mchezo ambao haukuchezwa baada ya Sudan kupeleka malalamiko yao kwa CECAFA na mchezo huo ukafutwa ambapo Vijana hao wanategemea kurejea nyumbani leo majira ya saa 2 za usiku.
NdextcuQurji Candice Hall https://wakelet.com/wake/-mYDe4qu6_zXvTgDsZ4O2
ReplyDeleteconttipslistsu