TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU TIMU YA KARUME BOYS ITATOLEWA KESHO


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo kesho inatarajia kutoa taarifa na ufafanuzi juu ya timu yake ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) ambayo imeondolewa kwenye Mashindano ya CECAFA U-17 yanayoendelea nchini Burundi.

Karume boys imeondolewa katika Mashindano hayo na kupigwa faini ya Dola 15000 pamoja na kufungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002. 

Katibu mkuu wa Wizara hiyo Omar Hassan (King) atatoa taarifa na ufafanuzi punde kesho majira ya Mchana katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Mjini Unguja ambapo Wizara hiyo itapokea Barua kutoka Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) .

Karume boys ilikuwa icheze jana mchezo wake wa kwanza dhidi ya Sudan katika uwanja wa Gitega mchezo ambao haukuchezwa baada ya Sudan kupeleka malalamiko yao kwa CECAFA na mchezo huo ukafutwa.

Wakati huo huo katika kundi A Ethiopia imenyanganywa ushindi dhidi ya Somalia kwasababu ya kuwachezesha wachezaji watatu waliozidi umri ambapo wachezaji hao watarejeshwa kwao kesho Jumanne.

Hivyo Wazanzibar kwa ujumla wasubiri taarifa ya Wizara kuhusu ufafanuzi wa tukio hilo na si kuongea na kutuma vitu vilivyokuwa havina uhakika bila ya kujua usahihi na ukweli wake.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS