ZFA ITAMWAGA MBOGA KESHO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU ZANZIBAR KUONDOLEWA KATIKA MASHINDANO YA CECAFA BURUNDI


Baada ya jana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo kutoa taarifa juu ya timu yake ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) ambayo imeondolewa kwenye Mashindano ya CECAFA U-17 yanayoendelea nchini Burundi, hatimae Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kimevunja ukimya na kesho kinatarajia kuongea na Waandishi wa Habari juu ya kadhia nzima iliyowakumba vijana wa Zanzibar nchini Burundi.

Mkutano huo utafanyika saa 4:00 za asubuhi katika ukumbi wa V.I.P wa uwanja wa Amaan ambapo viongozi wakuu wa chama hicho watakuwepo katika mkutano huo.

Jana Katibu mkuu wa Wizara ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo Omar Hassan (King) alisema ikithibitika kuwa ZFA wao ndio wenye makosa mpaka Karume Boys wakaondoshwa katika Mashindano basi wajiwajibishe.

Zanzibar imeondoshwa katika mashindano hayo na kupewa adahabu tatu ikiwemo kuondolewa katika mashindano, inaambatana na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni) zinazotakiwa kulipwa na Chama cha Soka la Zanzibar (ZFA), ambapo fedha hizo zitafidia gharama za tiketi, malazi na chakula ya timu katika kipindi chote walichokaa Burundi huku adhabu ya tatu ikiwa kufungiwa kutoshiriki mashindano yanayoendeshwa na CECAFA hadi hapo watakapolipa faini hiyo ambayo inatakiwa kurudishwa FIFA.
Kosa kubwa la Zanzibar katika Mashindano hayo ni kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo kanuni ya Mashindano hayo iliwataka wachezaji waliozaliwa kuanzia 01/01/2002 huku Zanzibar ikuwapeleka wachezaji 12 waliozaliwa 2001 jambo ambalo ZFA wamesema hawana taarifa kama wachezaji walotakiwa waliozaliwa 2002 ambapo wao walijuwa walokuwa na umri chini ya miaka 17 hivyo hata walozaliwa 2001 ikiwa bado hawajafika miaka 17.




Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS