KAMATI TENDAJI YA ZFA YAVUNJWA, WENGINE WAPYA KUCHUKUA NAFASI


Mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar ameufungia uongozi wa kamati tendaji ya ZFA ambao upo kwa mujibu katiba ya ZFA ya mwaka 2010 kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba yao.
Akizugumza na wandishi wa habari ukumbi wa uwanja wa Amani mjini Unguja Sleman Pandu Kweleza amesema ofisi ya mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar imefanya hivyo kwa mujibu wa sheria kwa kuwa ndio wanao simamia vyama vya michezo vyote Zanzibar.
Akitoa sababu ya kufungia kamati hiyo mrajisi Pandu Kweleza amesema baada ya kushindwa na kuupuza ombi la mrajisi la kutaka badhi ya vifungu vya katiba yao ya ZFA kufanya marekebisho na kushindwa kufanya hivyo, aidha mrajisi amefafanua alindakia barua kamati tendaji ya ZFA tarehe 20/3/2018 yenye kumbu kumbu no BTMZ /MRJS/ VOLUME/10 ya kutaka kufanya marekibisho baadhi ya maeneo ya katiba ya ZFA.
Aidha kwa upande mwengine mrajisi amesema kamati tendaji ya ZFA imeshindwa kusimamia kanuni za michezo na kusababisha ligi kuu ya Zanzibar kuonekana haina mvuto na kuzorota kwa mpira wa Zanzibar na kuupuza amri ya mahakama kuu ya Zanzibar mwaka 2014 ya kutaka chama hicho kubadilisha katiba na kuwa na Katiba inayoendana na CAF, ili kuondosha migogoro isiyo ya lazima.
“Niliwapa muda kufanya marekibisho toka tarehe 20 mwezi wa tatu hadi tarehe 20/5 na kushindwa kufanya marekibisho lakini kamati hiyo ilipuuza ombi la mrajisi ambaye ni msimamizi wa katiba za vyama vya michezo” Alisema Kweleza.
Hata hivyo mrajisi Kweleza ameteua kamati tendaji nyengine itakayosimamia majukumu ya kamati tendaji ya ZFA kwa mujibu wa katiba ya ZFA inayoundwa na wajumbe wafuatao :
Mwalim Ali Mwalim (Mwenyekiti).
Khamisi Abdalla Saidi ( Katibu).
Muhamed Hilali Muhamed (Katibu msaidizi).
Yussuf Muhamed Ali (Mjumbe).
Rajabu Juma Mtumweni (Mjumbe).
Mzee Ali Muhamedi (Mjumbe).
Abdulghani Abdalla Saidi (Mjumbe).
Kweleza amesema kamati hiyo mpya tendaji ya muda itatekeleza majukumu yake kama yalivyoanishwa kwenye katiba ya ZFA aidha mrajisi amesema kamati hiyo itatekeleza majukumu ya kusimamia upatikanaji wa Katiba mpya ya ZFA, kusimamia mashindano yote zilizochini ya ZFA ikiwemo nane bora ya ligi kuu ya Zanzibar.
Aidha mrajisi amemalizia kwa kusema viongozi wa wilaya watendelea na majukumu yao ya kawaida ila watakuwa chini ya kamati tendaji mpya.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS