LIGI KUU ZANZIBAR MSIMU WA MWAKA 2017-2018 KUENDELEA TENA KESHO


Ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya nane bora msimu wa mwaka 2017-2018 inatarajiwa kuanza rasmi kesho kwa kupigwa michezo miwili katika Viwanja viwili tofauti majira ya saa 10:00 za jioni.

Katika uwanja wa Amaan wataanza kucheza timu ya JKU dhidi ya Zimamoto ambapo katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba Mwenge wataivaa timu ya Jamhuri.

Hatua hiyo ndio itakayotoa Bingwa na Makamo Bingwa wa Zanzibar watakaowakilisha Zanzibar katika Mashindano ya Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo timu nne za Unguja zilizofanikiwa kutinga hapo ni JKU (Mabingwa Watetezi), Zimamoto (Makamo Bingwa), Mafunzo na KVZ huku kwa upande wa Kanda ya Pemba ni Jamhuri, Mwenge Opec na Hardrock.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS