ZFA YATOA KALENDA YA MWAKA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Teule ya Chama Cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA), imetoa kalenda ya msimu mpya wa mashindano na matukio mbali ya mchezo huo wa Soka kwa msimu wa mwaka 2018-2019.

Kalenda inaonyesha kuanza na zoezi kwa vilabu kuwasilisha Majina ya wachezaji walioachwa  ambapo zoezi hilo tayari limeshaanza tangu Septemba 1 hadi 15 mwaka huu 2018.

Kuanzia tarehe 16-27/09/2018 zoezi la uhamisho wa Wachezaji linaanza ambapo kuanzia tarehe 28/09/2018-05/10/2018 zoezi la usajili kwa Wachezaji litachukua nafasi wakati kuanzia tarehe 01-05/10/2018 itakuwa kipindi cha Refresh Course.

Kwa mujibu wa Kalenda hiyo, kuanzia tarehe 06-10/10/2018 itakuwa ni siku za Pingamizi ya Usajili ambapo tarehe 10-15/10/2018 kutakuwa na zoezi la Copa Test kwa Waamuzi na Mafunzo ya Leseni kwa Vilabu.

Tarehe 11-17/10/2018 ni siku za kupitia fomu na kutoa block Registration.

Mchezo wa Ngao ya Jamii utachezwa tarehe 18/10/2018 ambapo ligi za madara yote yataanza kuanzia tarehe 20/10/2018.

Tarehe 01/11/2018 Maandalizi ya timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwaajili ya Mashindano ya Cecafa Senior Challenge Cup.

Tarehe 01-18/12/2018 Michuano ya Cecafa Senior Challenge Cup.

Tarehe 10/12/2018 Maandalizi ya Kombe la Mapinduzi.

Tarehe 25/12/2018 Mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu kumalizika.

Tarehe 28/12/2018-13/01/2019 Michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Tarehe 01-20/01/2019 Mapumziko ya Dirisha Dogo na Uhamisho.

Tarehe 21-25/01/2019 Usajili wa Dirisha Dogo.

Tarehe 26/01/2019-05/02/2019 Kupitia Fomu za Usajili na Kutoa Block Registration .

Tarehe 06/02/2019-29/05/2019 Kuendelea ligi mzunguko wa Pili.

Tarehe 01/03/2019-30/05/2019 FA Cup na Ligi za Mabingwa wa Wilaya Daraja la Pili.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS