JABIR AENGULIWA, HUSSEIN AHMADA AKUBALI YAISHE UCHAGUZI WA ZFF

Mkurugenzi wa Ufundi wa Kamati ya Olympik Tanzania (TOS), Suleiman Mahmoud Jabir, ambae alikuwa anagombea nafasi ya urais kwenye Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) ameondoshwa katika kinyang'anyiro hicho kwa kile kilichoelezwa kukiuka taratibu za uchaguzi kwa kufanya kampeni kabla ya muda.
Akizungumza na Kisanduzenj Makamo mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Juma Msafiri Karibona amesema Jabir wamemuondosha kwenye orodha ya wagombea nafasi ya Urais kutokana na kwenda kinyume na masharti yaliyowekwa na kamati inayosimamia uchaguzi huo huku Hussein Ahmad Vuai ambae alikuwa anagombea nafasi ya Makamo wa Urais amejitowa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro hicho.
‘’Mgombea Suleiman Mahmoud tumemuondowa kwasababu kakosa sifa kwa vile tumejiridhisha kaanza kufanya kampeni za kimakundi kabla ya muda wa kampeni, na hoja ya pili tumegunduwa   hana maadili mazuri, kwaiyo barua yake tayari tumeshampa na tumemtoa rasmi’’.
Tulimtafuta Suleiman Mahmoud baada ya kuondolewa kwenye mchakato huo amesema amesikitishwa na kamati hiyo kumuundoa kwenye uchaguzi huo.
‘’ Kwa kweli nasikitika kuona nchi yangu imenisomesha kwa mapenzi na mimi juhudi zangu za kuendeleza masuala haya ya michezo hasa ngazi ya uongozi, ati sina sifa wakati nimekuwa najulikana hapa Afrika na nje ya Afrika kwenye masuala haya ya uongozi wa michezo, nimepokea barua ati inasema nimeaanza kampeni! Barua hiyo haina ushahidi wowote ati nimeanza kampeni, barua haina ushahidi ya kusema kuna kikao kilifanywa au tarehe Fulani, muda Fulani na watu Fulani nimepiga kampeni, hahahhaha yani inachekesha sana’’. Alisema Suleiman.

Wagombea waliopitishwa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa ngazi Rais ni Khamis Abdallah Said, Ame Abdallah Dunia na Seif Kombo Pandu wakati wanaowania nafasi ya Makamo ni Khamis Shaali Chum na Salum Ubwa Nassor ambapo Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika June 2, 2019 Kisiwani Unguja na sasa rasmi kampeni zimefunguliwa.


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS