SOKA LA ZANZIBAR LAPATA UONGOZI MPYA, SEIF BOSS ASHINDA UCHAGUZI WA ZFF

Kushoto rais mpya wa ZFF Seif Kombo Pandu, wa kati ni Khamis Abdallah Said na kulia ni Ame Abdallah Dunia walikuwa wagombea Urais ZFA

Kilio cha wadau wa soka wa Zanzibar cha kutaka kufanyika uchaguzi mkuu ndani ya shirikisho la mpira wa miguu Zanzibar kimemalizika baada ya kamati ya uchaguzi  iliopewa jukumu kukamilisha zoezi hilo.

Uchaguzi huo ambao umefanyika leo katika ukumbi wa makao makuu ya chuo cha Mafunzo Kilimani mjini Unguja, wajumbe wa mkutano mkuu wamemchagua Seif Kombo Pandu kuwa rais wa shirikisho hilo kwa  mara ya kwanza baada ya kupata asilimia 57 ya kura zilizopigwa kwa kujikusanyia kura 16 kati ya kura 28.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwenye uchaguzi wa ZFF

Kiti hicho cha urais ambacho kiligombaniwa na wajumbe watatu ambapo Seif Kombo  amechukuwa urais huwo baada ya kuwapita wapinzani wake Ame Abdalla Dunia aliepata kura tano na Khamis Said Abdalla aliepata kura 7.

Hata hivyo wajumbe hao wamemchagua Salum Ubwa Nassor kuwa makmo wa rais  wa shirikisho hilo kwa kupata asilimia 89 kati ya kura zote zilizopigwa na kumpita mgombea mwenzake Khamis Shaali Chuom ambae alipata kura tatu kwenye kura 28.


Ali Othman (Kibichwa) Rais wa Jangombe Boys 
Pia wajumbe wa mkutano huo  wamepata fursa ya kuwachagua  wajumbe wa kamati tendaji kutoka mikoa yote mitano ya Zanzibar.

Waliopata nafasi hizo za kuwa wajumbe wa kamati tendaji ni Seif Muhammed Seif mkoa wa kusini Pemba, Omar Ahmed Awadhi Kaskazin Pemba, Seif Bausi Nassor Kaskazin Unguja , Suleiman Haji Hassan Mjini magharibi na Salum Ali Haji Kusini Unguja.
Ali Ussi Bakar (Jongo) Katibu wa timu ya Zimamoto

Mwenyekiti wa uchaguzi huo Fadhil Ramadhan Mberwa amesema uchaguzi huo ulikuwa huru kwani umefata taratibu na sheria zote za  Uchaguzi.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS