TIMU ZA ZANZIBAR ZIMEAANZA VYEMA MASHINDANO YA UMISSETA


MASHINDANO ya umoja wa michezo kwa skuli za sekondari Tanzania Umisseta, yameanza kutimia vumbi katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Ufundi Mkoani Mtwara, huku Zanzibar ikianza kwa kishindo michezo hiyo.

Katika Mashindano hayo timu ya mpira wa kikapu ya kanda ya Pemba imetoka na ushindi wa vikapu 36 -15 dhidi ya Singida huku Unguja nayo mpira wa Kikapu imeanza kwa kishindo baada ya kuichapa Kigoma vikapu 38-23.

Kwa upande wa mpira wa Wavu timu ya Kanda ya Pemba imetoka na ushindi wa seti 3-1 dhidi ya Mara kwa wanawake na wanaume Pemba ikakubali kichapo cha seti 3-0 dhidi ya Ruvuma ambapo Unguja Wavu ikachapwa na Mbeya kwa seti 3-1.

Katika Soka Zanzibar haikuanza vizuri baada ya Unguja kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Dodoma huku Pemba wakichapwa 3-1 na Katavi ambapo mpira wa Pete Unguja ikifungwa na Dodoma mabao 21-12.


Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS