UFAFANUZI JUU YA MCHEZAJI SHAIBU NINJA KUSAJILIWA MAREKANI LA GALAXY



Wadau wengi wa Soka hapa Zanzibar na Tanzania Bara wanahamu sana kujua juu ya hatma ya Beki wa zamani wa Yanga Abdalla Haji Shaibu (Ninja) kuhusu kwenda kucheza Soka nchini Marekani.

Ni kweli Ninja sasa yupo Marekani kwenye timu ya La Galaxy ambapo amekwenda kwa mkopo, na baada ya kufanyiwa vipimo vya afya na mambo mengine La Galaxy wamelazimika kumuweka timu ya La Galaxy II (Timu B) na baada ya kuonekana anahitaji kuzowea mazingira na kupata uzoefu kidogo kwenye timu hiyo B kisha watampandisha kucheza timu kubwa ambayo inashiriki ligi kuu Soka Marekani, timu ambayo anacheza Zlatan Ibramovic.

Ninja tayari ameshaanza mazoezi kwenye timu hiyo B na uzuri kwamba timu hiyo B wakati mwengine wanachanganyika kufanya mazoezi na timu kubwa kwasababu muda wowote mchezaji wa timu B akionyesha kiwango hupandishwa timu kubwa.

Ninja amepewa jezi no 51, hivyo naomba Watanzania wafahamu kuwa kijana wao alikusudiwa kwenda kwa mkopo kwenye timu kubwa lakini kutokana na kutofanya mazoezi kipindi kirefu tangu kumaliza ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita Mei 28, 2019 mpaka juzi anafika Marekani hakuwa fit kucheza timu ya Primier kwani kwani zaidi ya miezi mitatu hakufanya mazoezi imara ya pamoja na ukiangalia ligi ya Marekani inaendelea.

Naomba tena Watanzania wafahamu Ninja amesajiliwa Timu a MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech barani Ulaya kwa mkataba wa miaka 4 lakini timu yake hiyo ambayo inashiriki ligi Daraja la Tatu nchini humo ndiyo imemtoa kwa mkopo wa mwaka mmoja kwenda kucheza kwenye klabu ya LA Galaxy Marekani lakini sivyo tulivyotegemea acheze LA Galaxy ambayo inashiriki ligi kuu Soka ya Marekani (MSL) ikiwa na nyota kadhaa waliyowika Duniani akiwemo mchezaji wa zamani wa Barcelona, Inter Milan na Manchester United Zlatan Ibrahimovic, ila mambo yamekwenda vyengine kidogo kwa kuekwa timu B.


Naomba niwafahamishe tena Watanzania timu B si timu ndogo, timu B ina thamani kubwa sana kwani wakati wowote kukilazimika kuongezwa mchezaji anapandishwa na wakati mwengine wanafanya mazoezi na timu kubwa hivyo si hatua ndogo Ninja kutoka Yanga mpaka kucheza La Galaxy II nchini Marekani na kubwa ni kumuombea dua afanikiwe kwani akifanikiwa yeye ndio kutufungulia njia Watanzania wengine kupata nafasi.
Kwa wale ambao wanasema Ninja hajaenda La Galaxy ya Marekani wafunguwe link hiyo wataona La Galaxy wenyewe walivyomuweka

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS