Posts

Showing posts from May, 2017

KIKOSI CHA UMISSETA KANDA YA UNGUJA KITAKACHOKWENDA MWANZA KIMEPATIKANA

Image
Kocha msaidizi wa timu ya soka Kanda ya Unguja Abdul wahab Dau “Mwalimu Dau” ametangaza kikosi kipya wachezaji 21 cha timu hiyo ambacho kinatarajiwa kwenda Butimba Jijini Mwanza  katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA)yanayotarajiwa kuanza  June 6, 2017. Kikosi hicho kinatarajia kuondoka Visiwani Zanzibar siku ya Jumamosi ya June 3, 2017. WALINDA MLANGO Aley Ali Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu) WALINZI Ibrahim Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi (Glorious), Abubakar Khamis (Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali Issa Omar (Lumumba),  Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki) na Abbas Yahya. VIUNGO Amani Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess” (Lumumba), Haji Suleiman (JKU Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku “Ozil” (Kinuni) na Eliyasa Suleiman (K-pura). WASHAMBULIAJI Faki Kombo (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan (Bububu), Walid Abdi “P...

KOMBAIN YA MJINI YA ROLLING STONE YAZIDI KUSUKWA UPYA, SASA WAPO 30 WA UHAKIKA AKIWEMO ABUU LUIZ WA CITY

Image
Mabingwa  watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone kombain ya Mjini Unguja ambayo  inaandaliwa na Kocha Mohammed Seif “King” kwenda jijini Arusha kwenye Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kuanzia June 29, 2017 na kumalizika July 9, 2017. Kwa mujibu wa kocha King uteuzi wa kuchagua wachezaji umefikia tamati na hakuna atakaengezwa tena baada ya kufika jumla ya Wachezaji 30 ambapo watachujwa 6 na kubakia 24 ambao ndio watakaokwenda katika Mashindano hayo. Wachezaji 30 ni :-   WALINDA MLANGO  Aley Ali Suleiman “Manula” (Miembeni city), Peter Dotto Mashauri (Schalke 04), Makame Mkadar Koyo (Huru) na Ibrahim Abdallah Ali “Parapanda” (Amani Fresh). WALINZI WA PEMBENI Muharami Khamis “Terra” (Black Sailors), Abdul hamid Salum “Ramos” (KVZ), Hassan Chalii (Kipanga), Abdul-halim Ameir (King Boys), Ali Hassan (Uhamiaji), WALINZI WA KATI Ali Juma Maarifa “Mabata” (Taifa ya Jang’ombe), Shaa...

RAZA LEE AWAPA TAFU MABINGWA WATETEZI WA ROLLING STONE

Image
Mwana michezo Mohd Ibrahim “Raza Lee” ambae ni mtoto wa Mbunge wa Jimbo la Kiemba Samaki Ibrahim Raza asubuhi ya leo ameisaidia mipira timu ya kombain ya Mjini Unguja ambao ni Mabingwa  watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone, Mashindano ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi June 29, 2017 na kumalizika July 9, 2017 jijini Arusha. Mipira hiyo Raza Lee ameikabidhi timu hiyo Dukani kwake ambalo ni Duka la Vifaa vya Michezo ambapo Ali Othman “Kibichwa” Meneja wa Timu hiyo pamoja na Mohammed Seif “King” kocha wa timu hiyo ndio waliyopokea Mipira hiyo. Mohd Ibrahim "Raza Lee" akiwakabidhi Mipira Ali Othman "Kibichwa" Meneja na Mohammed Seif "King" Kocha

WADAU WAIJIA JUU RASIMU YA KATIBA YA ZFA, WENGINE WANA HOJI KWANINI MBUNGE AJUWE KUSOMA NA KUANDIKA WAO MPAKA WAWE NA FORM IV?, NA KWANINI IANDIKWE KWA KIENGEREZA?

Image
Baadhi ya wadau wa Soka Visiwani Zanzibar wameijia juu Rasimu ya awali ya katiba ya ZFA iliyowasilishwa hivi karibuni kwa kusema kuna vipengele havifai kabisa kuwemo na kwanini katibu na Mwenyekiti wa ZFA Wilaya awe na elimu kuanzia kidato cha nne wakati huo huo wakihoji kwanini iandikwe kwa lugha ya Kiengereza wakati wao ni Waswahili na wanatumia lugha yao ya Kiswahili. Wakizungumza wakati tofauti na Mtandao huu baadhi ya Viongozi wa ZFA Wilaya ambao hawakupenda majina yao kutajwa wamesema ni vigumu sana kupita rasimu hiyo kwani ina mapungufu mengi sana. “Hii Rasimu ina vichekesho sana tulipoiona tulishtuka, sisi viongozi ati tuwe na elimu kuanzia Form IV, kisha imeandikwa kwa Kiengereza wakati sisi ni Waswahili!, si rahisi kupita mazali na sisi ni miongoni mwa wapitishaji, kwasababu uongozi si kusoma bali uongozi ni kipaji na mapenzi ya kitu”. Juzi Jumatatu ya Mei 29, 2017 Kamati ya kuandika upya katiba ya ZFA chini ya katibu wao Saleh Ali Said iliwasilisha rasimu ya...

BAZA KUMEKUCHA WAJIPANGA KUFANYA UCHAGUZI JUNE, WATAKA KUTEKELEZA AGIZO LA BTMZ

Image
Kikosi cha Mafunzo cha Basket ball Chama cha Mpira wa Kikapu Zanzibar  “BAZA” kipo mbioni kufanya Uchaguzi wake ambao unatarajiwa kufanyika Mwezi wa June, 2017 ambapo mpaka sasa haujajulikanwa utafanyika tarehe gani. Akizungumza na Mtandao huu wa kisanduzenj.blogspot.com makamo mwenyekiti wa BAZA Rashid Hamza amesema kwasasa wapo katika harakati za kufanya uchaguzi wao ambao utafanyika mwishoni mwa mwezi wa June mwaka huu. “Sasa tupo mbioni kufanya uchaguzi, na uchaguzi wetu tunatarajia kufanya ndani ya mwezi wa sita, kwasasa tunaendelea na mchakato huo na mambo yanakwenda vizuri mpaka muda huu”. Alisema Hamza. Hivi karibuni BARAZA la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), limeviagiza vyama vya michezo  ambavyo havijafanya uchaguzi  kufanya hivyo ili kupata viongozi kulingana na katiba zao ili waongoze kwa demokrasia na kwa kufuata katiba. Vyama vitano (5) ambavyo vinaharakishwa kufanya uchaguzi ndani ya mwezi June, 2017 ni Chama cha Basketball Zanzibar ...

MWENGINE WA SERENGETI BOYS HUSSEIN DECO APIGA HODI MJINI UNGUJA, SASA WAMEPANIA KUTETEA TAJI LAO LA ROLLING STONE

Image
Mabingwa  watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone kombain ya Mjini Unguja wamepania kutetea taji lao baada ya kuzidi kuimarisha kikosi chao kufuatia ujio wa kiungo mshambuliaji wa timu ya Kilimani City Assad Juma “Hussein Deco” ambae asubuhi ya leo kwenye uwanja wa Amaan ameanza mazoezi. Hussein Deco  amerejea Visiwani Zanzibar hivi karibuni akitokea mjini Gentil, nchini Gabon katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya AFCON akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania “Serengeti Boys” baada ya kutolewa kwa kufungwa 1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, nchini Gabon. Huyo ni mchezaji wa pili kwenye timu hiyo ya Mjini Unguja mwenye uzoefu wa kucheza mashindano makubwa ya AFCON kufuatia juzi   Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” kujumuika na wenzake hao ambao  wanatarajia kwenda jijini Arusha mwezi July mwaka huu kwenye Mashindano ya Vijana ya Rolling S...

MUANDISHI WA BOMBA FM APATA BONGE LA SHAVU

Image
Suleiman Ussi Haji “Mido” ambae ni muandishi na mtayarishaji wa kipindi cha michezo cha SPORTS BOMBA cha Bomba FM amechaguliwa kuwa afisa Habari wa Kamati ya Soka Ufukweni visiwani Zanzibar. Mara baada ya Chama cha Soka Visiwani Zanzibar kupata uanachama wa kudumu wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” wakaitaka Kamati ya soka la ufukweni kuunda uongozi mpya ambao rasmi kwasasa umewekwa hadharani. Uongozi huo ambao unaongozwa na Ali Sharifu “Adolf” ambae ni Mwenyekiti, Katibu Fahad Khamis, mshika fedha Hassan Ali Mzee, mjumbe Ali Omar Abdallah huku Muhsin Ali “Kamara” na Mohd Rajab ni washauri wa kamati hiyo ambapo Afisa Habari ni Suleiman Ussi Haji “Mido” . Tayari kamati hiyo imeshapata baraka zote kutoka ZFA taifa na imepania kuanza rasmi majukumu yake.

MLINDA MLANGO NAMBA MOJA WA MIEMBENI CITY ASEMA KAZI WALOTUMWA NA VIONGOZI WAO WAMESHAMALIZA ZAMANI, WANACHOSUBIRI KUCHEZA LIGI KUU

Image
Golikipa mahiri wa timu ya Miembeni City Aley Ali Suleiman “Manula” amesema mzigo waloagizwa tayari wameshaufikisha panapostahiki wanachosubiri sasa ni kucheza ligi kuu soka ya Zanzibar msimu ujao. Mbali ya kuwa mabingwa City lakini bado hawana uhakika wa kucheza ligi kuu msimu ujao ambapo Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” kimepania kuchezesha vilabu 12 tu pekee kwenye ligi kuu msimu huo, wakati huo huo mpaka sasa vipo vilabu 28. Timu hizo 28 ni zile 12 za Unguja na 12 za Pemba zilizobakia msimu huu, na nyengine 2 za Unguja na 2 za Pemba zilizotoka Daraja la Kwanza, ndipo hapo kwa pamoja watapanga ni mfumo gani utumike ili zipatikane timu 12 za msimu ujao ambapo mpaka sasa inasubiriwa imalizike 8 bora ndipo mchakato huo uanze. Aley amesema wao kama wachezaji walitumwa wafanye kazi kuipandisha timu daraja na tayari wameshafanya hivyo, kilichobakia wanasubiri ZFA wataamua vipi kuhusu vilabu 12 vitakavyocheza ligi kuu msimu ujao. “Sisi wachezaji tushafanya kazi tuliyo...

MLINZI KINDA WA TAIFA YA JANG’OMBE AJUMUISHWA KWENYE KIKOSI CHA ROLLING STONE

Image
Mlinzi wa kati wa Timu ya Taifa ya Jang’ombe Ali Juma Maarifa “Mabata” amejumuishwa kwenye kikosi cha kombain ya Mjini Unguja ambacho kinajiandaa na Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone yanayotarajiwa kufanyika mwezi July mwaka huu jijini Arusha. Mabata ni miongoni mwa walinzi wadogo wanaocheza ligi kuu soka ya Zanzibar lakini shughuli yake uwanjani tofauti na umri wake ambapo miaka yake chini ya miaka 17 ataungana na wachezaji wengine wa kombain hiyo inayofundishwa na kocha Mohammed Seif “King”. Nyota wengine waliyoitwa hivi karibuni kwenye kikosi hicho ni Ibrahim Abdallah Ali “Mkoko” wa Miembeni ambae hivi karibuni amerejea Visiwani Zanzibar akitokea mjini Gentil, Gabon katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya AFCON akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania “Serengeti Boys” baada ya kutolewa kwa kufungwa 1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, nchini Gabon. Wengine ni Aley Ali Suleiman “Manula” Mlinda mlan...

KIKOSI CHA UMISSETA KANDA YA UNGUJA CHAWEKWA HADHARANI, JUNE 3 WATAENDA MWANZA

Image
Kocha msaidizi wa timu ya soka Kanda ya Unguja Abdul wahab Dau “Mwalimu Dau” ametangaza kikosi kipya wachezaji 22 cha timu hiyo ambacho kinatarajiwa kwenda Butimba Jijini Mwanza  katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA)yanayotarajiwa kuanza  June 6, 2017. Wachezaji hao 22 watachujwa 4 na kubakia 18 ambao watakaokwenda katika Mashindano, mchujo wa mwisho unatarajiwa kufanywa siku chache kabla ya safari. Kikosi hicho cha wachezaji 22 wa kanda ya Unguja Walinda mlango ni:- Aley Ali Suleiman (Ubago) na Abass Wadi (Philter) Wachezaji wengine ni Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki), Amani Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ali Mohd Seif (Tumekuja), Ali Issa (Lumumba), Jamali Ali Jaku (Kinuni), Elias Suleiman (K-pura) na Abdurahman Seif Bausi (Glorious). Wengine ni Ibrahim Faraj (Lumumba), Faki Kombo (JKU Mtoni), Haji Suleiman (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan (Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Walid Abd...

MSHAMBULIAJI WA SERENGETI BOYS AJUMUISHWA KATIKA KIKOSI CHA MJINI UNGUJA, ALIPORUDI GABON TU AFCON KOCHA KING AMDAKA, LEO AANZA MAZOEZI NA WENZAKE

Image
Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” asubuhi ya leo ameungana na wachezaji wa kombain ya Mjini Unguja kwenye mazoezi katika Uwanja wa Amaan kwa kujiandaa na Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone yanayotarajiwa kuanyika mwezi July mwaka huu jijini Arusha. Mkoko amerejea Visiwani Zanzibar juzi akitokea mjini Gentil, Gabon katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya AFCON akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania “Serengeti Boys” baada ya kutolewa kwa kufungwa 1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, nchini Gabon. Mara baada ya kumaliza mazoezi asubuhi ya leo Mtandao wa kisanduzenj.blogspot.com umefanya mahojiano na mshambuliaji huyo kwa kuelezea kujiunga na timu hiyo ya Mjini. “Nimefurahi kuona kuwa bado Wanzibar na Watanzania wana imani na mimi, nilipowasili tu Zanzibar kutokea Gabon nkapigiwa simu na kocha King nije kujiunga na timu ya Mjini Unguja, nimefurahi sana na leo nimejiunga ...

BAADA YA ZU KUSHINDA KOMBE LA ZAHILFE, UWANJA WA AMAN UKAFURIKA MASHABIKI KATI KATI YA UWANJA

Image
JANA Chuo cha Zanzibar University (ZU) wamefanikiwa kutetea taji lao baada ya kuwafunga Afya Mbweni mabao 4-1 katika fainali ya tano ya Mashindano ya Vyuo Vikuu na taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar (ZAHILFE CUP) katika uwanja wa Amaan. Lakini punde tu Muamuzi wa Pambano hilo Mfaume Ali Nassor kupuliza penga kuashiria mchezo huo kumalizika Mashabiki wakaingia uwanjani kushangiria ushindi huo. HISTORIA YA ZAHILFE 2013  AFYA MBWENI PENALTI 5-4 ZU, DAKIKA 90 WALITOKA 0-0 2014 CHWAKA PENALTI 5-4 ZITOD, DAKIKA 90 WALITOKA 1-1 2015 SUMAIT 1-0 ZU 2016 ZU 4-2 CHWAKA 2017 ZU 4-1 AFYA

ZU MABINGWA TENA ZAHILFE

Image
Chuo cha Zanzibar University (ZU) wamefanikiwa kutetea taji lao baada ya kuwafunga Afya Mbweni mabao 4-1 katika fainali ya tano ya Mashindano ya Vyuo Vikuu na taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar (ZAHILFE CUP) katika uwanja wa Amaan. Mabao ya ZU yamefungwa na Hassan Hemed dakika ya 10 na 43, Nabil Amour (Jaja)  dakika 35 na Yussuf Haji dakika ya 51. Bao pekee la Afya limefungwa na Yakoub Omar dakika ya 41. HISTORIA YA ZAHILFE 2013  AFYA MBWENI PENALTI 5-4 ZU, DAKIKA 90 WALITOKA 0-0 2014 CHWAKA PENALTI 5-4 ZITOD, DAKIKA 90 WALITOKA 1-1 2015 SUMAIT 1-0 ZU 2016 ZU 4-2 CHWAKA 2017 ZU 4-1 AFYA

LIVE, ZU WANAONGOZA 4-1 DHIDI YA AFYA, FAINALI YA ZAHILFE CUP

Image
Zanzibar University (ZU) 4-1 Afya Mbweni. Fainali ya tano ya Mashindano ya Vyuo Vikuu na taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar (ZAHILFE CUP) katika uwanja wa Amaan. Mabao ya ZU yamefungwa na Hassan Hemed dakika ya 10 na 43, Nabil Amour (Jaja)  dakika 35 na Yussuf Haji dakika ya 51. Bao pekee la Afya limefungwa na Yakoub Omar dakika ya 41. Mpira umeisha ZU mabingwa.

ZU YAONGOZA KUCHEZA FAINALI MARA NYINGI ZAHILFE CUP, KESHO KISASI CHENGINE KWA AFYA, ANGALIA HISTORIA YA TIMU ZILIZOTINGA FAINALI MIAKA YOTE

Image
Fainali ya Mashindano ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar (ZAHILFE CUP) inatarajiwa kusukumwa kesho majira ya saa 10:00 za jioni kwenye uwanja wa Amaan kati ya Mabingwa wa watetezi wa Mashindano hayo Chuo cha Zanzibar Univeristy (ZU) dhidi ya Chuo cha Afya Mbweni. Historia ya Mashindano hayo ambayo kwasasa ni Mashindano ya 5 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013, ZU ndio timu iliyocheza mara nyingi fainali baada ya kucheza mara 3 na kufungwa mara mbili wakishinda mara 1 ambapo kesho itakuwa fainali yao ya 4 kucheza katika Mashindano hayo. Bado rikodi zinaonesha kuwa ZU ni Chuo Bora baada ya kufika fainali miaka yote isipokuwa mwaka mmoja (2014) kwenye miaka 5 ya Mashindano hayo. Afya Mbweni hii ni mara ya pili kufika fainali kufuatia mwaka 2013 kuwafunga ZU bao 1-0 ambapo kesho ZU anataka kulipa kisasi huku Afya wanataka kuendeleza kuwafunga tena fainali ZU. HISTORIA YA ZAHILFE 2013  AFYA MBWENI PENALTI 5-4 ZU, D AKIKA 90 WALITOKA 0-0 2014 CHWAKA PE...

HONGERA MZENJ KOCHA BUSHIR KUISAIDIA MWADUI KUSHINDA TUZO TIMU YENYE NIDHAMU

Image
Timu yenye nidhamu kwenye ligi kuu msimu uliomalizika ni Mwadui FC ya Shinyanga ambayo imepata zawadi ya Sh. 17.5 milioni. Timu hiyo inafundishwa na Mzanzibar Ali Bushir "Bush" ambae alitoka KMKM ya Zanzibar. Bush kwenye ufundishaji wake huwa yupo makini na nidhamu tangu alipokuwa Mlinda Mlango wakati alipokuwa akicheza mpaka kuwa Mwalimu na leo timu yake imefanikiwa kuwa ndio timu pekee yenye nidhamu kwenye timu 16 zilizoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2016-2017. Blog hii inampongeza kocha Bush.

JANG’OMBE BOYS YAPATA SHAVU KUCHEZA SPORTPESA SUPER CUP, WATASHINDANA NA KINA YANGA, SIMBA, SINGIDA UNITED, GOR MAHIA, NAKURU ALL STAR NA LEOPARD

Image
Timu ya Soka ya Jang’ombe Boys inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar imepata bahati ya kuwemo kwenye Mashindano ya  Sport Pesa Cup yanayotarajiwa kuanza kutimu vumbi June 5, 2017 jijini Dar es salam. Ligi hiyo itashirikisha jumla ya timu 8 kutoka Tanzania na Kenya ambayo itachezwa kutafuta bingwa na mshindi wa pili. “Ni kweli kwa hapa Zanzibar Jang’ombe Boys pekee wamepata mualiko kucheza Ligi hiyo ambayo itahusisha vilabu vikubwa vya Bara na Kenya”. Kilieleza chanzo. RATIBA KAMILI HIYO 5/6/2017 Singida united Vs FC leopard Yanga Vs Tusker fc 6/6/2017 Simba Vs Nakuru All Star Jang`ombe boys vs Gor mahia Nusu fainali tarehe 8/6/2017 Bingwa wa mechi kati ya Singida united vs AFC leopard atacheza na bingwa kati ya Yanga na Tusker. Nusu fainali ya pili Bingwa wa mechi kati ya Simba na Nakuru all-star atacheza na bingwa wa mechi kati ya Jangombe boyz na Gor mahia Fainali ni tarehe 11/6/2017 ambapo Bingwa wa SportPesa Super Cup ataondok...

COCA-COLA YAZIPIGA JEKI SHULE ZA SEKONDARI ZANZIBAR KWA KUWAPATIA JEZI NA MIPIRA

Image
Kampuni ya vinyaji baridi ya Cocacola imetoa Vifaa vya Michezo vikiwemo jezi na mipira kwa ajili ya Skuli za Sekondari 251 za Unguja na Pemba kwa ajili ya michezo ya soka na mpira wa kikapu, pamoja na mashindano ya UMISSETA ambayo yatakayofanyika kuanzia June 6, 2017 huko Butimba Mkoani Mwanza ambapo Zanzibar mwaka  huu zitatoa kanda mbili tofauti, Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba. Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Waziri wa Habari, Utalii, Utamduni na Michezo Rashid Ali Juma ambae ndie aliyekuwa mgeni rasmi na ameipongeza kampuni hiyo kwa kuthamini Michezo huku akisisitiza kuvithamini na kuvitunza vifaa hivyo. Mbali ya Vifaa hivyo pia Kampuni hiyo imetoa Vinywaji vya Coca cola kwa Wanafunzi na Wananchi wote waliyofika Uwanjani hapo Amaan kwenye hafla hiyo. Afisa masoko msaidizi wa kampuni ya Cocacola Pamela Lugenge

LUMUMBA YAPIGWA NA UMISSETA MBELE YA MKURUGENZI WA MICHEZO WIZARA YA ELIMU

Image
Kikosi cha UMISSETA Unguja Katika kujiweka sawa na Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) timu ya Kanda ya Unguja imecheza mchezo wa kirafiki na timu ya Shule ya Lumumba katika Uwanja wa Amaan asubuhi ambapo timu ya UMISSETA ya Unguja ikafanikiwa kuibuka na Ushindi wa Mabao 3-1. Mabao ya Kombain ya UMISSETA yamefungwa na Ali Mohd dakika ya 4 na 50, na jengine likifungwa na Iliyasa Suleiman dakika ya 26. Bao pekee la Lumumba limefungwa na Ali Assaa dakika ya 32. Kikosi cha Shule ya Lumumba Hassan Tawakal Khairallah Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar akiwasalimia timu ya UMISSETA Kanda ya Unguja. Mashindano ya UMISSETA yanatarajiwa kuanza June 6, 2017 huko Butimba Mkoani Mwanza ambapo Zanzibar mwaka huu zitatoa kanda mbili tofauti, Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.

BONAZA LA MASAUNI CUP USIPIME MWAKA HUU

Image
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania (Aliyevaa kofia) ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Kikwajuni Hamad Yussuf Masauni akizikabidhi Jezi kwa kamati ya Mashindano ya Masauni na Jazira CUP, Mashindano ambayo yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan baada ya Sala ya Tarawehe.  Endelea kufatilia Blog hii itakuletea taarifa zote kuhusu Mashindano hayo zikiwemo Ratiba, Timu shiriki, Zawadi kwa Washindi na mambo mengi kuhusu Bonanza hilo. Hamad Yussuf Masauni 

WALE WALOCHUKUA UBINGWA WA ROLLING STONE MWAKA JANA MJINI UNGUJA KUWAPA MAZOEZI NDUGU ZAO KOMBAIN MPYA YA MWAKA HUU KWA KUCHEZA MCHEZO MAALUM WA KIRAFIKI

Image
Mabingwa wa mwaka jana katika Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati (Rolling Stone) Timu ya Mjini Unguja watacheza mchezo maalum wa kirafiki na ndugu zao ambao wamechaguliwa kuunda timu ya Mjini Unguja msimu huu itakayokwenda kucheza Mashindano hayo mwezi July mwaka huu jijini Arusha, mchezo huo utapigwa kesho Alhamis majira ya saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Amaan. Mnamo tarehe 9 July, 2016 siku ya Jumamosi timu hiyo ya Mjini Zanzibar ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Rolling stone kwa mara ya Kwanza ndani ya miaka 15 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya DAREDA ya Mkoani Manyara katika uwanja wa SHEIKH AMRI ABEID mjini Arusha. Mabao ya Zanzibar Mjini siku hiyo yalifungwa na Ali Humud “Balii” dakika 42 na Hafidh Barik “Fii” dakika ya 44 huku bao pekee la DAREDA likifungwa na Najim Mussa dakika ya 83. Timu hiyo ina Jumla ya wachezaji 22 ambao msimu huu wote wameachwa akibakishwa mmoja tu ambae ni Abdul rahman Juma “Baby” ambapo kesho watacheza mech...

AMOUR JANJA ATOKEA BENCHI NA KUPELEKA MSIBA JANG’OMBE BOYS

Image
Na: Mossi Abdallah, Zanzibar. Ligi kuu ya Zanzibar hatua ya 8 bora jioni ya leo imemaliza mzunguko wa 3 kwenye dimba la Amaan ambapo Timu ya JKU imefanikiwa kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jang’ombe Boys. Mchezo huo ambao ulikuwa mgumu kwa timu zote mbili na kupelekea hadi mapumzika hakuna timu iliyoona lango la mwenziwe. Kurudi kumaliza kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kwa kila upande kutaka kuondoka na alama tatu muhimu lakini mchezaji aliyetokea benchi Amour Omar “Janja” akaipatia alama tatu JKU baada ya kufunga bao katika dakika ya 89 ya mchezo. Ligi hiyo itakwenda mapumziko kupisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kisha kuendelea mzunguko wa nne ambapo mpaka sasa Jamhuri ndie kinara mwenye alama 9 kufuatia kushinda michezo yake yote mitatu ya awali. Wachezaji wa JKU

ILE MECHI ILIYOSHINDWA KUMALIZWA JANA PENALTI BAADA YA KUINGIA GIZA, HATIMAE LEO IMEMALIZWA KWA KUPIGWA PENALTI MOJA TU NA IPA KUUNGANA NA ZU, AFYA NA ZIFA NUSU FAINALI ZAHILFE

Image
Timu ya soka ya Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar (IPA) leo imetinga hatua ya nusu fainali kwenye Mashindano ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar baada ya kushinda penalty 1-0 dhidi ya SUMAIT kufuatia mchezo huo kuendelezwa mchana wa leo kwenye dimba la Amaan. Mchezo huo ni muendelezo kufuatia jana kutoka sare ya 2-2 ndani ya dakika ya 90 katika uwanja wa Fuoni kisha kupigiana mikwaju ya penalti 6 na kutoka sare ya 5-5 kufuatia kila timu kukosa penalti1 na kupata 5. Pambano likalazimika kulazwa jana na kuendelezwa leo kwa mikwaju ya penalti na iliendelea penalti moja moja kwa kila timu ambapo SUMAIT walikosa na IPA wakapata, hivyo IPA wametinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya penalti 6-5. Nusu fainali ya Mashindano hayo zitapigwa kesho majira ya saa 10:00 za jioni katika Viwanja Viwili tofauti. Katika uwanja wa ZU Tunguu watasukumana kati ya Chuo cha Afya Mbweni dhidi ya IPA, na katika uwanja wa Fuoni ZU mabingwa watetezi watakipiga na ZIFA ambao ni ...

WAZANZIBAR TUMUOMBEE DUA MOHAMMED BANKA KESHO KUSHINDA TUNZO YA MCHEZAJI CHIPUKIZI LIGI KUU TANZANIA BARA 2016/17

Image
Kiungo wa Timu ya Mtibwa Sugar Mohammed Issa  “Banka” wengine wanamfamu kwa jina la Mudy Gold ambae ni Mzanzibar amefanikiwa kuingia kwenye orodha ya majina matatu ya wachezaji wanaogombea tunzo ya mchezaji bora anayechipukia kwenye ligi kuu soka Tanzani bara ambayo imehitimishwa Jumamosi iliyopita. Banka ameonesha kiwango cha hali ya juu akicheza kwa mara ya kwanza ligi kuu soka Tanzani bara msimu huu ambapo alitokea klabu ya Chuoni Visiwani Zanzibar ambapo amechaguliwa kuwemo kwenye kinyanganyiro cha tunzo hiyo. Sherehe za Tunzo hizo zitafanyika  kesho Jumatano Mei 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wachezaji wengine ambao wanawania tunzo hiyo ni Mbaraka ABEID wa Kagera Sugar na Shaaban IDD wa Azam FC. Mtandao wa kisanduzenj.blogspot.com umemtafuta kiungo huyo ambae kwasasa yupo hapa kwao Visiwani Zanzibar na kusema kuwa amefurahishwa mno kuwemo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tunzo hiyo ikiwa yeye ndio mara yake ya kwan...