MLANDEGE HOI KWA AMAN FRESH, KESHO KWEREKWE CITY NA GULIONI
Mchezo wa kwanza hatua ya 4 bora ligi daraja la pili Wilaya ya Mjini kati ya Mlandege dhidi ya Aman Fresh wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 1-1 mchezo uliopigwa saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan. Aman Fresh ndio wa mwanzo kupata bao katika dakika ya 51 kupitia Rashid Suleiman Said. Bao la Mlandege limefungwa kwa penalti na Saleh Salum "Neymar" dakika ya 86. Lakini munamo dakika ya 63 Mohd Abdallah "Edi Mundo" wa Mlandege alikosa penalti. Mchezo mwengine utapigwa kesho Mei Mosi kati ya Gulion na Kwerekwe City mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan. Mchezo huo ni wa kulipana kisasi kwani msimu huu timu hizo zilikutana Jumapili ya Disemba 4, 2016 katika hatua ya Makundi ambapo Gulioni alipigwa mabao 5-0 dhidi ya City, sasa sijui kesho itakuaje Gulioni atalipa kisasi au City ataendeleza ubabe. Bingwa na Makamo Bingwa katika ligi hiyo watawakilisha Wilaya ya Mjini kwenda kucheza na Wilaya nyengine sita zikiwemo...