Posts

Showing posts from June, 2017

JKU ACADEMY YAPANIA KUCHUKUA UBINGWA WA ROLLING STONE, MAPEMA WANATANGULIA ARUSHA KUZOWEA BARIDI

Image
Timu za JKU Academy zimepania kubeba ubingwa wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati (Rolling Stone) ambapo mwaka huu wakitarajia kushiriki timu tatu tofauti katika Mashindano hayo ikiwemo timu chini ya miaka 13, 15 na 17 ambapo msafara wa watu 60 ukitarajiwa kuondoka Visiwani Zanzibar Jumapili usiku July 2, 2017. Msafara huo ambao utajumuisha timu tatu tofauti za JKU Academy pamoja na waamuzi wao vijana watano na viongozi watano. Mtandao huu umemtafuta Khatib Omar Salum ambae ni kocha mkuu wa JKU Academy na ametuelezea mchakato mzima wa safari yao kwenda huko na maandalizi yao walivyojipanga. “Jumapili tunatarajia kuondoka Zanzibar, tunategemea Jumatatu tuanze safari ya Arusha na tutafika Jumatatu usiku, tunaenda mapema ili tuzowee mazingira ya baridi lakini pia mimi naamini tutabeba vikombe mwaka huu, tuna timu tatu n azote zipo vizuri sana mwaka huu”. Alisema. Mashindano ya Rolling Stone mwaka huu yanatarajiwa kuanza rasmi July 9 na kumalizika July 19...

KLABU YA KOREA KUCHEZA NA TAIFA YA JANG’OMBE

Image
Kikosi cha Hallelujah FC Klabu ya Halelujah FC inayoshiriki ligi daraja la Pili Korea ya kusini kesho Jumamosi July 1, 2017 itacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Jang’ombe ambayo inashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar, mchezo huo utapigwa majira ya saa 9:30 ya Alaasir katika uwanja wa  Amaan. Katika mchezo huo hakutokuwa na kiingilio chochote ambapo Wakorea wenyewe watatoa tiketi bure kwa mashabiki wote watakaofika Uwanjani hapo. Mchezo mwengine wa kirafiki timu ya Halelujah FC itacheza na timu ya Polisi ya Zanzibar inayoshiriki ligi kuu, mchezo ambao utasukumwa Jumanne July 4, 2017 saa 9:30 Alaasir katika uwanja wa Amaan. Hallelujah FC imeanzishwa December 20, 1980 huko kwao Korea ya Kusini ambapo jana waliwasili hapa Visiwani Zanzibar kwaajili ya kufanya ziara maalum pamoja na kupata mazoezi kwa kucheza na baadhi ya vilabu vya Zanzibar. Kikosi cha Taifa ya Jang'ombe

MAJESHI WA TANZANIA WAPANIA KUFANYA KWELI MASHINDANO YA MAJESHI YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Image
Timu za michezo mbali mbali za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zimepania kutwaa ubingwa katika Mashindano ya Majeshi ya Afrika Mashariki na Kati Mashindano ambayo mwaka huu yatafanyika Bujumbura Mjini Burundi mwanzoni mwa mwezi Agost. Akizungumza na Mtandao huu Kanal Mwandike ambae ni Mkurugenzi wa Michezo wa JWTZ amesema wamepania kufanya kweli mwaka huu ambapo matayarisho ya Mashindano hayo yanaendelea vizuri na sasa wapo kambi Visiwani Zanzibar kwa kujiandaa na Mashindano hayo. Amesema lengo lao mwaka huu kubeba kombe hilo ambapo mwaka jana walichukua nafasi ya pili katika Mashindano hayo. “Mwaka huu tumepania kufanya vyema kuliko mwaka jana, mana mwaka jana tulishinda nafasi ya pili, tupo hapa Zanzibar kwaajili ya Maandalizi na tumepania kufanya kweli mwaka huu”. Alisema Kanal Mwandike. Mashindano ya Majeshi ya Afrika Mashariki na Kati hufanyika kila mwaka, ambapo mwaka huu Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litashiriki kwa michezo mitano ikiwemo mpir...

HAPATOSHI LEO USIKU AMAN

Image

HUYU MLINZI KINDA HATARI WA REAL KIDS, JANA KAKABA ULINZI TAIFA NOWMA, SAMIR AMPA TANO

Image
Zanzibar ni Visiwa vyenye vipaji vingi sana ambapo kila siku vinaibuka vyengine vipya, tukija kwenye soka sitaki kuongea sana lakini jana kama umeangalia mchezo wa kirafiki kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Gulioni katika uwanja wa Amaan, bila ya shaka umemuona kinda jipya limefunga mlango kwenye safu ya ulinzi ya Taifa, si mwengine bali ni Ibrahim Abdallah ni beki wa kati wa timu ya Real Kids inayoshiriki ligi za madaraja ya vijana wilaya ya Mjini, lakini jana alitumiwa na Taifa na alivaa jezi nambari 29 mgongoni. Ibrahim unaweza ukamuona ni mlinzi wa kawaida lakini huyu dogo ni nowma hata Samir Yahya beki wa kati wa Taifa ya Jang’ombe amekubali kazi yake jana na kusema huyu mtoto hatari. “Nime enjoy sana leo kucheza na Ibra katikati, dogo ana kibaji na anauwezo, anakuja vizuri sana naamini akizidi kucheza atakuwa bonge la beki hapa Zanzibar, nimefurahi sana na huwenda akawa mrithi wa Ninja au hata mimi nikiondoka basi naamini dogo ataziba pengo bila ya wasi wasi, kuna vitu...

ZAIDI YA MAKOCHA 30 KUSHIRIKI KOZI YA MAGOLIKIPA ZANZIBAR

Image
Mkufunzi Saleh Ahmed Seif "Machupa" Kozi ya awali ya makocha wa Magilikipa Visiwani Zanzibar inatarajiwa kufanyika July 5 na kumalizika July 11, 2017 chini ya Mkufunzi Gwiji  Saleh Ahmed Seif “Machupa”. Kozi hiyo imeandaliwa na Chama cha Soka Zanzibar “ZFA” ambayo itawashirikisha zaidi ya makocha 30 kutoka Unguja na Pemba na makocha hao wakimaliza kozi hiyo watapata fursa ya kutambuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF”. Mtandao huu umemtafuta Mkufunzi huyo Machupa na kutaka kujua matayarisho yanaendeleaje ya Kozi hiyo ambapo amesema kila kitu kipo sawa mpaka sasa na yeye baada ya kuhitimu kozi ya Ukufunzi aliagizwa na CAF kuendesha kozi popote nchini Tanzania. “Matayarisho yanaendelea vizuri mpaka sasa, mimi niliagizwa na CAF niendeshe kozi kama hizi maana makocha wengi wanafundisha lakini hawana taaluma ya ukocha wa makipa”. Alisema Machupa. Machupa ni Mkufunzi pekee nchini Tanzania aliyehitimu Kozi ya CAF ya Wakufunzi wa Makocha wa Magolikipa...

KESHO NI ZAMU YA BOYS NA GULIONI SHEREHE ZA KUFUNGA SIKUKUU ZA EID

Image
Kikosi cha Gulion FC Timu ya Gulioni FC bado inaendelea na mchakato wake wa kujiweka sawa kucheza ligi Daraja la Kwanza Taifa Unguja msimu mpya ambapo kesho Alhamis Iddi nne watacheza mchezo mwengine wa kirafiki na timu ya Jang’ombe boys, mchezo ambao utasukumwa saa 2:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan. Gulioni jana walipigwa 2-1 na Taifa ya Jang’ombe katika mchezo wa kirafiki ambapo kesho wamepania kufuta makosa yao mbele ya Boys. Viingilio vya mchezo huo ni Shilingi 2000/=, 3000/= na  VIP 5000/= . Kikosi cha Jang'ombe Boys

TAIFA YAJIFARIJI SIKUKUU KWA GULIONI

Image
Timu ya Taifa ya Jang'ombe imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gulioni katika mchezo maalum wa kirafiki uliosukumwa leo saa 3 za usiku katika uwanja wa Amaan. Mabao ya Taifa yamefungwa na Omar Chande na Adam Ibrahim "Edo" wakati bao pekee la Gulioni limefungwa na Amour Pwina. Gulioni wanatarajia kucheza mchezo mwengine wa kirafiki siku ya Alhamis Iddi Nne dhidi ya Jang'ombe boys saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan.

BONGE LA GAME KESHO

Image

GULIONI NA TAIFA YA JANG’OMBE KUNOGESHA SIKUU YA EID PILI KESHO AMAN

Image
Katika kusheherekea Sikuu ya Eid Fitir timu ya Taifa ya Jang’ombe na Gulioni watacheza mchezo maalum wa kirafiki kesho Jumanne Iddi Pili mchezo ambao utasukumwa majira ya saa 2:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan. Viingilio vya mchezo huo ni Shilingi 2000/=, 3000/= na  VIP 5000/= . Mbali ya mchezo huo kesho, siku ya Alhamis Iddi nne Gulioni watacheza mchezo mwengine wa kirafiki dhidi ya Jang’ombe Boys mchezo ambao utapigwa majira ya saa 2:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan.

“KILA MTU ANAWEZA NA HAKUNA KUKATA TAMAA HATA WAZANZIBAR WANAWEZA KUCHEZA LIVERPOOL” - MAMADOU SAKHO

Image
Sakho na watoto wake akiwa pamoja na mmiliki wa blog hii Abubakar Khatib (Kisandu) Katika Maisha hakuna kukata tamaa hasa kwa Vijana kwani hakuna kisichowezekana katika Dunia hii, hayo si maneno yangu bali ni maneno ya beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England wakati alipokuwa akiangalia mpira katika Visiwani Zanzibar katika Uwanja wa Aman kwenye mchezo maalum wa uzinduzi wa COCO SPORTS NDONDO CUP ambapo Taifa ya Jang’ombe walipigwa 2-1 na Mlandege. Amesema ni kosa kwa kijana kukata tamaa kwani akiweka malengo na kujituma atatimiza ndoto zake. “Ukiwa na malengo kisha ukajituma zaidi basi unaweza kutimiza ndoto zako, kwa wachezaji wa hapa Zanzibar hata Liverpool wanaweza kucheza lakini wakiwa na malengo yao na kujituma, hakuna kisichowezekana, mimi napenda kuona vijana hawakati tamaa”. Aidha Sakho amefurahishwa mno katika mchezo huo kwenye uwanja wa Amaan huku akisema kuwa ame enjoy sana mapumziko yake Visiwani Zanzibar huku akisema m...

MAMADOU SAKHO- “BABAANGU ALIKUFA NIKIWA NA MIAKA 12 NA MAISHA YALIKUWA MAGUMU MNO, SASA NINA UWEZO NA MUNGU ATANIULIZA PESA ZANGU NIMEZITUMIA VIPI? LAZIMA NIWASAIDIE WANYONGE

Image
Sakho na familia yake wakipiga picha ya pamoja na watoto yatima wa SOS Leo Saa 8 za mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ataondoka Beki wa kimataifa wa Ufaransa na kurejea nyumbani, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England ambae alikuwepo Visiwani Zanzibar tangu Jumamosi ya June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja kufika hapa Zenj. Lakini mchezaji huyo anaondoka Zanzibar kwa kuwacha ujumbe mzito kwa Wazanzibar baada ya kusema kuwa yeye ni tajiri na anauwezo mkubwa sana lakini binafsi yake anajua fika kuwa akifariki Mwenyezi Mungu atamuuliza utajiri wake ameutumia vipi? Amesema yeye anauwezo mkubwa wa fedha na muumini wa Dini ya Kiislamu hivyo Mungu atamuuliza fedha zake amezitumia kwa njia gani.   Watoto Yatima wa kituo cha SOS wakimsubiri Sakho katika kijiji chao Mombasa Unguja “Mimi fedha ninazo nyingi sana na lakini najua f...

MATUKIO KWA PICHA YA SAKHO WA LIVERPOL ALIPOWATEMBELA WATOTO YATIMA ZANZIBAR

Image
Mfaransa Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England jana jioni  alitembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS kilichopo Mombasa Unguja.   Sakho amefatana na mke wake Madna na Watoto wake wawili wa kike. Watoto Yatima wa kituo cha SOS Mombasa Unguja wakimpokea Sakho Sakho akisalimiana na wanakijiji cha SOS ambao ni watoto Yatima Sakho akisalimiana na wanakijiji cha SOS ambao ni watoto Yatima Vijana nao hawapo nyuma kupiga picha za kumbukumbu Picha ya pamoja Sakho na watoto Yatima wa SOS Baadhi ya Vyakula alivyotowa msaada Sakho kwenye kituo cha SOS

GULIONI WANAKUJA KIVYENGINE MSIMU HUU, KWANZA WANAANZA NA TAIFA KISHA BOYS

Image
Timu ya Soka ya Gulioni FC inayoshiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini imepania kuwatia michezo miwili ya kirafiki kwenye sherehe za Sikuu ya Eid pili na nne ambapo Eid Pili watasukumana na Taifa ya Jang’ombe kisha Eid nne kucheza na Jang’ombe boys mechi zote zitachezwa saa 2:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan. Akizungumza na Mtandao huu Rais wa Gulioni Ahmed Khamis amesema maandalizi ya michezo hiyo yanaendelea vizuri na lengo lao ni kufanya mapinduzi ya soka la Zanzibar. “Tumejiandaa vizuri kucheza na Taifa Eid pili kisha Boys Eid nne lakini sisi lengo letu ni kuleta mapinduzi ya soka la Zanzibar”. Alisema Ahmed.

NINJA WA YANGA AWAAGA WAZANZIBAR, ATOA MANENO MAZITO KATIKA UWANJA WA AMAAN

Image
Mlinzi mpya wa Yanga Abdallah Haji Shaibu "Ninja" amewaaga mashabiki wa soka Visiwani Zanzibar na kuwaomba wamsamehe kama aliwakosea kwa kipindi chote alichocheza soka Visiwani hapa. Akiwaaga Mashabiki hao jana usiku katika uwanja wa Amaan kwenye mchezo maalum wa uzinduzi wa COCO SPORTS NDONDO CUP ambapo Taifa ya Jang’ombe walipigwa 2-1 na Mlandege, Ninja amewashukuru Makocha wake wote tangu alipokuwa mdogo mpaka kufika Taifa ya Jang’ombe. Aidha Ninja amewaomba Mashabiki hao wamsamehe kama aliwakosea kwa kipindi chote huku akiwataka wazidi kumuombe dua ili afanikiwe katika Maisha yake mapya ya Jangwani. “Kwanza Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kusajiliwa Yanga, la pili na nawashukuru Makocha wangu wote tangu walonifundisha kuanzia Juvenile, Junior na Central, la tatu nawashukuru Mashabiki wangu wa Taifa ya Jang’ombe kwa kunisapoti, na pia nawaomba Wazanzibar kama kuna mtu nimemkosea anisamehe na mimi nimeshawasamehe wote, hivyo muniombe pia dua kwa Mungu anisaidie...

TAIFA YAUKUBALI MZIKI WA MLANDEGE

Image
Mchezo wa kirafiki Taifa ya Jang'ombe 1-2  Mlandege katika uwanja wa Aman. Mabao ya Mlandege yamefungwa na Abdallah Edi Mundo dakika ya 60 na Razak Halfan dakika ya 78. Bao pekee la Taifa limefungwa na Ali Badru dakika ya 30.

SAKHO WA LIVERPOOL ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA ZANZIBAR

Image
Familia ya beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England jioni ya leo ametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS kilichopo Mombasa Unguja. Sakho amefatana na mke wake Madna na Watoto wake wawili wa kike. Leo Ijumaa saa 3:00 za usiku katika uwanja wa Amaan Sakho atazindua Mashindano ya COCO SPORTS NDONDO CUP katika uwanja wa Amaan, mchezo ambao watasukumana kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Mlandege SC. Sakho yupo hapa Viswani Zanzibar tangu Jumamosi June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja Jumamosi kufika hapa Zenj.

WALORATIBU SAFARI YA SAKHO WA LIVERPOOL ZANZIBAR 3:00 ZA ASUBUHI WATAZUNGUMZA NA COCONUT FM KUHUSU SAKHO KUFIKA AMAN LEO

Image
Kampuni ya Escapade Zanzibar Limited ambayo ndio Kampuni iliyompokea na kusimamia shughuli zote za ziara ya Nyota wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England, Kampuni hiyo itazungumza na Coconut FM 88.9 leo kuanzia saa 3:00 za asubuhi na kumuelezea mchezaji huyo kuhusu ujio wake wa kwenda kuzindua Mashindano ya COCO SPORTS NDONDO CUP katika uwanja wa Amaan, mchezo ambao watasukumana kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Mlandege SC leo kuanzia saa 3:00 za usiku. Sakho yupo hapa Viswani Zanzibar tangu Jumamosi June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja Jumamosi kufika hapa Zenj. Wapenzi wa soka watakaofika katika Uwanja wa Amani leo watapata fursa ya kumuona na wengine kupiga nae picha nyota huyo. Vingilio ni:- Tsh 2000 urusi Tsh 3000 wings Tsh 5000 V.I.P

SAKHO WA LIVERPOOL KUZINDUA NDONDO CUP YA COCONUT KESHO IJUMAA KATI YA TAIFA YA JANG'OMBE DHIDI YA MLANDEGE

Image
Beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England kesho Ijumaa saa 3:00 za usiku katika uwanja wa Amaan atazindua Mashindano ya COCO SPORTS NDONDO CUP katika uwanja wa Amaan, mchezo ambao watasukumana kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Mlandege SC. Sakho yupo hapa Viswani Zanzibar tangu Jumamosi June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja Jumamosi kufika hapa Zenj. Sakho amecheza mechi zaidi ya 200 katika klabu hiyo, akishinda nayo mataji yote manne ya nyumbani kabla ya mwaka 2013 kuuzwa Liverpool kwa dau la Pauni Milioni 18. Mwaka huu alitolewa kwa mkopo Crystal Palace pia ya Ligi Kuu England ambako amekwenda kucheza mechi nane. Sakho ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha wakubwa cha Ufaransa, ambaye awali amechezea timu zote za vijana na za nchi hiyo. Tangu acheze mechi yake ya kwanza kikosi cha wakubwa cha Ufaransa mwaka 2010 dhidi ya England, Sakho ame...

KESHO NI MLANDEGE NA TAIFA MECHI MAALUM YA KUMUAGA NINJA ALIYESAJILIWA YANGA

Image
KESHO Ijumaa ya June 23, 2017 Saa 3:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan Mlinzi mpya wa Yanga Abdallah Haji Shaibu "Ninja" atawaaga Mashabiki wake katika mchezo maalum kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi Mlandege SC mchezo ambao pia ni wa uzinduzi wa COCO SPORTS NDONDO CUP. Ninja amesajiliwa Yanga wiki iliyopita akitokea Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar ambapo amefunga mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo na kesho atapata fursa kubwa ya kuwaaga Mashabiki wake. Kiingilio katika mchezo huo ni Shilingi Elfu 2000/=, 3000/=  na VIP 5000/=.

MAKUNDI YA UJIRANI MWEMA NDONDO CUP YAWEKWA HADHARANI

Image
Mashindano ya ujirani mwema Ndondo CUP inatarajiwa kuanza rasmi mnamo July 9, 2017 katika uwanja wa Maungani kati ya Mabingwa watetezi timu ya Miembeni dhidi ya Microtech ambapo Kamati ya Mashindano hayo pia imepanga makundi 4 katika timu 20 zitakazocheza. KUNDI A Miembeni, Kane Kombain, Birmingham, FC Lugalo na Microtech. KUNDI B Qatar, Kilimani City, Kikungwi, No Fair na Tandale. KUNDI C African Coast, Njaa kali, Zantex na Unajua Unacheza na Nani. KUNDI D Jamaica, Oklahoma, Mitondooni, Daladala na Chaani Stars.  

CHARAWE WAKANUSHA KUUZA DARAJA, WASEMA HATA WAPEWE MILIONI 200 TIMU HAWAITOWI LENGO LAO KUCHEZA LIGI KUU NA KUCHUKUA UBINGWA

Image
Uongozi wa klabu ya Charawe Stars umekanusha taarifa za kuuza daraja kwa timu yao na kusema kuwa taarifa hizo si kweli na wao wapo katika maandalizi ya kucheza ligi kuu soka ya Zanzibar msimu ujao. Akizungumza na Mtandao huu  Ramadhan Abdallah “Sadifa” ambae ni msemaji wa timu hiyo amesema taarifa zilizozagaa mitaani ya kuwa timu yao imeuzwa sio kweli na kamwe hawawezi kufanya jambo hilo kwani ile ni timu ya Kijiji na lengo lao kucheza ligi kuu ndio mana wakapigana kufika hapo walipo. “Hizo taarifa sio kweli timu yetu hatuuzi wala haitouzwa, sisi tupo kwaajili ya kupambana kucheza ligi kuu ya Zanzibar, tunashukuru tumefanikiwa kutoka daraja la kwanza na kufika hapo tulipo kwasasa tunasubiri ligi kuu kucheza, hiyo timu inayosema inataka kununuwa nafsi yetu hata watuletee million 200 hatukubali, sisi tumepigana ndo mana tukafika ligi kuu na wao kama rahisi wapigane, sisi sio genge hii ni timu ya Wanakijiji, kama rahisi nawao wapigane wafike hapa tulipofika sisi, msimamo we...

BAADA YA KUKAA NJE YA SOKA ZAIDI YA MIAKA 10, KOCHA BURHAN MSOMA AELEZEA KILICHOMREJESHA, APANIA KULETA MABADILIKO YA SOKA LA ZANZIBAR

Image
Kocha wa zamani wa Simba, Kagera Sugar,Nairobi, Kenya Army, Fesal Sports Club, Forodha, Kikwajuni na Bandari, Burhan Msoma amerejea kwenye soka na sasa ni kocha mkuu wa klabu ya Gulioni FC inayoshiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini. Msoma ambae amefundisha soka kwa mafanikio hasa katika klabu ya Simba mwaka ya 2004 na kufanikiwa kufika hatua ya Robo fainali ya kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, ametoboa siri ya kurejea tena katika soka ambapo amesema siri kubwa baada ya kuona soka la Zanzibar limedorora ndipo alipoamua kurejea baada ya kushawishiwa na Gulioni. Amesema ameona soka la Zanzibar linazidi kupotea ndipo aliposhawishiwa na Abdul Mshangama kurejea tena nae akakubali ili akalikombowe ambapo amepania kulikomboa soka hilo. “Ni kweli nimekaa miaka mingi sana soka la Zanzibar silitaki hata kulisikia, lakini sababu kubwa ilonifanya nirejee kufundisha baada ya kushawishiwa na Abdul Mshangama kwenda kufundisha Gulioni, nikaamua bora nije kulikomboa s...

BOYS YABANWA NA WATOTO WA MJINI, WATAKIPIGA TENA LEO JIONI NA GULIONI

Image
Timu ya Soka ya Kombain ya Wilaya ya Mjini na Jang'ombe Boys zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0 katika mchezo maalum wa kirafiki uliosukumwa jana Jumatano saa 3 za usiku katika uwanja wa Amaan. Mjini watacheza mchezo mwengine wa kirafiki leo Alhamis kuanzia saa 10:15 za jioni dhidi ya timu ya Gulioni ambayo inashiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini. Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja kwa majukwaa ya kawaida na V.I.P ni shilingi Elfu mbili. Kombain ya Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017 huko Mburu Manyara wakati Jang'ombe boys wanajiandaa na kuendelea kucheza hatua ya 8 bora ligi kuu soka ya Zanzibar. Kikosi cha Gulioni

SEIFU TIOTE AWAOMBA WADAU WA SOKA KUISADIA KOMBAIN YA MJINI

Image
Kiungo mshambuliaji wa Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini Seifu Said Seifu (Tiote) amewaomba wadau wa soka Visiwani Zanzibar kuichangia timu yao ili wafanikishe safari yao ya kwenda Mburu Mkoani Manyara kushiriki Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone. Tiote ameyasema hayo wakati anazungumza na Mtandao asubuhi ya leo huku akisema mazoezi yanaendelea vizuri na wao wachezaji wana hamasa kubwa sana ya kutetea taji lao lakini wadau wa soka waisaidie timu yao ili ifanye vizuri kama msimu ulopita. “Mazoezi tunaendelea vizuri tuna hamasa kubwa sana mana tunakuja kwa wakati na tunapokea vizuri mafunzo ya walimu wetu lakini nawaomba wadau wa soka Zanzibar watuunge mkono kwa kutusaidia chochote ili tuweze kutetea taji mana hii timu inawakilisha Zanzibar nzima sasa”. Alisema Tiote. Mashindano ya Rolling Stone mwaka huu yatafanyika Mikoa miwili tofauti Arusha na Manyara kuanzia July 9 hadi July 19, 2017 ambapo kundi la Mjini Unguja ambao ndio mabingwa wat...

BAZA TAIFA UCHAGUZI JULY 9, WILAYANI JULY 1 NA JULY 4

Image
Chama cha Mpira wa Kikapu Zanzibar (BAZA) kinatarajia kufanya Uchaguzi wake ambao umepangwa kufanyika July 9, 2017. Katibu wa kamati ya Uchaguzi Kibabu Haji ametaja ratiba yote ya uchaguzi ambapo Uchaguzi huo unaanzia Wilayani na July 9 ukifanyika wa Taifa. Ratiba ya uchaguzi wa BAZA ngazi ya Taifa na wilaya kama ifuatavyo:- Kuanzia tarehe 14.6.2017 lilianza zoezi la Uchukuaji wa fomu ambapo tarehe 23.6.2017 ni siku ya mwisho ya urejeshaji wa fomu kwa wagombea wakati wa saa za kazi. Tarehe 24.6.2017 ni usaili wa wagombea baada ya kuthibitishwa kuwa mgombea anaruhusiwa kuanza kampeni na pingamizi kwa mgombea. Tarehe 01.7.2017 uchaguzi Wilaya Mjini  ambapo tarehe 04.7.207 ni uchaguzi Wilaya Chake .  Tarehe 09.7.2017 uchaguzi BAZA Taifa utafanyika Unguja.  Bei ya fomu kugombea nafasi za uongozi wilaya ni tsh 15,000/= na ngazi ya taifa tsh 40,000/= NAFASI ZINAZOGOMBANIWA WILAYA NI:- MWENYEKITI MAKAMO MWENYEKITI KATIBU MSHIKA FEDHA ...

JAN’GOMBE BOYS KUWAPA MAZOEZI KOMBAIN YA MJINI KESH

Image
Kikosi cha Jang'ombe Boys Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Jang'ombe Boys kesho  Jumatano saa 3 za usiku katika uwanja wa Amaan. Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja kwa majukwaa ya kawaida na V.I.P ni shilingi Elfu mbili. Kombain ya Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017 huko Mburu Manyara wakati Jang'ombe boys wanajiandaa na kuendelea kucheza hatua ya 8 bora ligi kuu soka ya Zanzibar.   Kombain ya Mjini

WAZANZIBAR WENGINE 2 KUTAKA KUSAJILIWA LIGI KUU BARA

Image
Kocha mkuu wa timu ya Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushir “Bush” amepania kufanya usajili wa wachezaji wa nne wapya kwa nafasi tofauti wakiwemo Wazanzibar wawili. Bushir amesema amepania kusajili wachezaji wa nne akiwemo Mlinda Mlango na Kiungo mkabaji kutoka Ligi kuu soka ya Zanzibar na wengine wawili ni Kiungo mshambuliaji na Mshambuliaji wa kati kutoka Ligi kuu soka ya Tanzania Bara. Amesema tayari ameshaanza mazungumzo na Wachezaji hao lakini kwasasa bado hajaweka wazi majina yao. “Nimepania kusajili wachezaji 4 tu katika dirisha hili, nafanya hivyo kwa vile wachezaji wangu wengi wameshanifahamu vyema taaluma yangu ndo mana ntasajili wa nne tu ili kuja kuongezea nguvu tu, wachezaji ambao nimeshaongea nao ni mlinda mlango na kiungo mkabaji kutoka ligi kuu ya Zanzibar, na wengine ni kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wa kati mmoja hawa wote kutoka ligi kuu ya bara, majina kwasasa sitowataja kwa vile nishapeleka ripoti kwa uongozi na binafsi nimeshaongea nao, Za...

KOMBAIN YA MJINI KUKIPIGA NA JANG'OMBE BOYS

Image
Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Jang'ombe Boys kesho kutwa Jumatano saa 3 za usiku katika uwanja wa Amaan. Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja na V.I.P ni shilingi Elfu mbili. Kombain ya Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017 huko Mburu Manyara wakati Jang'ombe boys wanajiandaa na kuendelea kucheza hatua ya 8 bora ligi kuu soka ya Zanzibar.

MFUMO UPI UTATUMIKA KUPATIKANA TIMU 12 ZA LIGI KUU MSIMU MPYA 2017-2018 UTAJULIKANA JULY 8, 2017 GOMBANI PEMBA

Image
Vilabu 28 ambavyo vimo katika mchakato wa upatikanaji wa timu 12 za ligi kuu soka ya Zanzibar msimu mpya wa mwaka 2017-2018 wametumiwa barua na Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kuhusu kikao cha mchakato wa upatikanaji wa timu kumi na mbili za ligi kuu msimu wa 2017-2018, kikao ambacho kitafanyika siku ya Jumamosi ya July 8, 2017 saa 3:00 za asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano wa uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba. Kwa mujibu wa barua hiyo viongozi wawili kwa kila klabu kati ya Vilabu 14 vya Unguja watahudumiwa na timu zao gharama zote za kwenda huko Pemba zikiwemo Usafiri, Kula na Malazi jambo ambalo kidogo limeleta mshtuko kwa timu hizo. Hayo yote yamekuja baada ya ZFA kuwa mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” ambapo moja ya agizo lao CAF ni kutaka msimu ujao wa mwaka 2017-2018 ligi kuu soka ya Zanzibar iwe na jumla ya timu 12 kwa Zanzibar nzima ambapo katika msimu huo wa mwaka 2016-2017 ulikuwa na jumla ya timu 36 kwa kila kanda ilikuwa ina timu 18,...

MWINYI HAJI- BADO KIDOGO NIJIUNGE NA SIMBA LAKINI MAPENZI YANGU NA JANGWANI NDIO YALOSABABISHA NIBAKIE YANGA

Image
Baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kukipiga na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga, mlinzi wa kushoto Mwinyi Haji Ngwali “Bagawai” ametoboa siri iliyomfanya kubakia Jangwani na kutokwenda Msimbazi licha ya kufatwa na Simba. Mwinyi amekiri kuongeza mkataba wa miaka miwili Yanga na pia aliweka wazi kuwa Simba walihitaji huduma yake lakini mapenzi yake Jangwani ndio sababu kubwa iliyomfanya kubakia Yanga. “Nimeongeza mkataba wa miaka 2 pale Yanga, na kweli Simba walinihitaji na mazungumzo yalikuwa yameshaanza na yamefikia pazuri sana, lakini bado naipenda Yanga yangu ndio mana nimebakia Jangwani”. Alisema Mwinyi.